Best African Low-Cost Airline Africas leading low cost airline 2016 winner shield Book Direct for the Lowest fares

Uhakika wa bei kwenye mtandao Nunua tiketi yako moja kwa moja kupitia www.fastjet.com kwa ajili ya kuepuka ada za ziada

Vifaa vya michezo

Unaruhusiwa kubeba vifaa vya michezo ila hauruhusiwi kuchanganya vifaa vya michezo pamoja na nguo za kawaida.

Ubebaji unatolewa kwa

 • Baiskeli
 • Vifaa vya kuchezea gofu (Isipokuwa viatu vya kuchezea gofu)
 • Vifaa vya michezo ya baharini
 • Silaha za moto
 • Wanyama 
 • Vifaa vya kuchezea upepo (parachuti)
 • Vifaa vya kuogelea majini (gesi na mitungi yake hairuhusiwi)

Gharama za nyongeza za US$ 38 kwa kila kifaa kwa gharama za kawaida ya 20kg. Angalia jedwali la gharama na ada na pia hairuhusiwi kuzidisha 32kg.

Maelezo zaidi- Baiskeli

Baiskeli inatakiwa kuhifadhiwa katika box au begi. Pia begi moja linatakiwa kuwa na baiskeli moja. Hairuhusiwi kubeba mzigo wa aina yoyote katika box au begi la baiskeli mfano nguo. Tairi zanatakiwa kuchomolewa na mishikio kufunguliwa ili iendane na box na vinyongeo kuingizwa ndani au kutolewa.

Kwa wateja wenye kusafiri na mzigo wa baiskeli wanatakiwa kuwasili kabla ya masaa mawili ndege kuondoka.

Kiwango cha kibadilisha fedha kitakachotumika kuanzia 01/12/2015 ni US$ 1 = TZS 2,200; ZAR 15; UGX 4,000; ZMW 14; MWK 600, KES 110.

Mizigo inayoruhusiwa

Kitu chochote kikubwa zaidi ya begi la mkononi (56x45x25sm) inatakiwa kukaguliwa kama mzigo.

Kwa safari za ndani ya Tanzania: Begi moja lenye lisilizidi kilo 20 kwa abiria inaruhusiwa kwa gharama ya US$ 10 kama italipiwa kabla ya siku ya kuondoka, US$ 25 italipiwa uwanja wa ndege siku ya safari.

Kwa safari za kimataifa: kwa mabegi mawili  yenye uzito usiozidi kilo 20 kila moja litakaguliwa kwa gharama ya US$ 15 kama ikilipwa kabla ya siku ya kuondoka na US$ 30 kama ikilipwa uwanja wa ndege siku ya safari.

Abiria watakao kuwa na kilo zaidi ya 40 watanunua kwanza “shehena” na kilo 80 zitachajiwa US$ 80.

Hakutakuwa na marejesho ya pesa au malipo ya awali endapo uzito wa begi lako utakuwa pungufu ya uzito uliolipiwa.

Kama utahitaji zaidi ya kilo 20 hii itapangwa uwanja wa ndege kwa gharama ya US$ 6 kwa kilo. Tafadhali kumbuka uzito wa juu kabisa kwa kila mzigo mmoja ni kilo 32, Hii ni kutokana na sheria za usalama na kiafya.

Kuongeza mzigo kwenye tiketi yako, tafadhali ingia Manage my Booking/ Manunuzi yangu ya tiketi kwenye tovuti yetu, piga huduma kwa wateja au temebelea moja ya vituo vyetu vya mauzo.

Kiwango cha kibadilisha fedha kitakachotumika kuanzia 01/12/2015 ni US$ 1 = TZS 2,200; ZAR 15; UGX 4,000; ZMW 14; MWK 600, KES 110.

Mizigo inayoruhusiwa kubebwa mkononi

Mteja anaruhusiwa kubeba mzigo mmoja mkononi wenye ukubwa usiozidi 56 x 45 x 25sm, mfano sanduku dogo, mkoba, au kibegi cha kubebea nguo. Haina haja ya kupima uzito wa mzigo huo ila unatakiwa kuhakikisha mzigo wako unakaa sawa katika sehemu ya kuhifadhia mzigo huo.

Kumbuka, watoto chini ya miaka miwili wanaofsafiri bila kukatiwa tiketi hawaruhusiwi kubebewa mizigo.

Iwapo mzigo wako utazidi kiwango kilichotajwa hapo juu  wakati wa kuingia au wakati wa kutoka  na gharama za kuzidisha mzigo zitatozwa.

Kuanzia tar 1 Februari 2015, fastjet ikitekeleza matakwa ya South Africa Civil Aviation, itaruhusu abiria kubeba begi moja la mkononi lisilozidi kilo 7 kwa safari za kutoka Johanesburg kuelekea Dar es Salaam.

Wanyama

Ubebaji wa wanyama, wadudu, mifugo hauruhusiwi.

Vifaa vya muziki

Vifaa vya muziki vinaweza kubebwa kama begi ya mkononi kutegemeana na uzito wa kifaa hicho na inatakiwa iwe ni mzigo mmoja.

Vifaa hivyo vinatakiwa kuwa na ukubwa wa 30 x 117 x 38sm. Vifaa vyenye ukubwa zaidi ya huo vitatunzwa sehemu ya kutunzia mizigo.

Gitaa la muziki linaweza kuingia na kubebwa ndani ya ndege endapo kiti kwa ajili yake itakuwa imelipiwa. Unafuu huu hauruhusiwi kwa vifaa vingine zaidi ya zaidi ya gitaa bila kujali ukubwa au udogo wake kwa sababu za kiusalama wa ndege.

Hakikisha unachunga vifaa vyako ili kuepuka kupotea au kuharibika. Kwa maelezo zaidi juu ya ubebaji wa mizigo, tafadhali wasiliana na watoaji huduma wetu.

Silaha za moto

Bastola zinaweza kubebwa katika safari zote za mtandao wa fastjet. Hakuna malipo kwa ajili ya kubeba bastola.

Bunduki za michezo au mashindano zinabebwa kwa gharama ya US$ 38 kwa kila moja inategemea na vigezo hapo chini.

 • Abiria (wenye umri zaidi ya miaka 18 tu) lazima aonyeshe nyaraka halali za kuthibitisha umiliki na mamlaka ya kisheria ya kumiliki silaha ya moto. Bila ya hizo nyaraka, silaha hiyo HAITABEBWA.
 • Silaha za moto zipo chini ya Polisi na taratibu za kiusalama, hivyo unashauriwa kufika uwanja wa ndege saa 2 kabla ya muda wa ndege kuondoka.
 • Bunduki lazima ziwekwe kwenye kisanduku kigumu cha kusafiria ambacho kinafungika.
 • Risasi zisizozidi kilo 5 zinaweza pia kubebwa, endapo zitakuwa zimepakiwa ndani ya mzigo mwingine unaoingia chini ya ndege.

Viwango vya kubadilishia fedha za kigeni kama ilivyokuwa 01/12/2015: US$ 1 = TZS 2,200; ZAR 15; UGX 4,000; ZMW 14, MWK 600, KES 110.