Best African Low-Cost Airline Africas leading low cost airline 2016 winner shield Book Direct for the Lowest fares

Uhakika wa bei kwenye mtandao Nunua tiketi yako moja kwa moja kupitia www.fastjet.com kwa ajili ya kuepuka ada za ziada

Vigezo na Masharti

Usafiri wote na fastjet unazingatia vigezo na masharti yetu ya uchukuzi.

Yaliyomo

 1. Kifungu cha 1. Ufafanuzi
 2. Kifungu cha 2.Kutumika
 3. Kifungu cha 3. Tiketi
 4. Kifungu cha 4. Nauli, Kodi, Ada
 5. Kifungu cha 5. Kuweka nafasi
 6. Kifungu cha 6. Kuunganisha
 7. Kifungu cha 7. Ukaguzi na Kupanda ndege
 8. Kifungu cha 8. Kikomo cha Mizigo
 9. Kifungu cha 9. Mizigo
 10. Kifungu cha 10. Kuchelewa na Kufuta safari
 11. Kifungu cha 11. Kurudisha fedha
 12. Kifungu cha 12. Jumla
 13. Kifungu cha 13. Mipango
 14. Kifungu cha 14. Taratibu za kiutawala
 15. Kifungu cha 15. Dhima ya Madhara
 16. Kifungu cha 16. Kikomo cha muda wa madai
 17. Kifungu cha 17. Masharti Mengine
 18. Kifungu cha 18. Tafsiri

1. MANENO NA MISAMIATI ILIYOTUMIKA KATIKA MASHARTI HAYA

Usomapo masharti haya, tafadhali zingatia kwamba:

Maneno “Sisi”, “yetu” na “sisi binafsi” yanamaanisha Shirika la ndege la fastjet likifanya biashara kama fastjet. Maneno “wewe", “yako/yenu”, na “wewe/nyie binafsi” yanamaanisha mtu yeyote/msafiri, isipokuwa mmoja wa wafanyakazi wa ndege, aliyebebwa au atakayebebwa kwenye ndege kulingana na tiketi.

 “Number ya Utambulisho wa Ndege” inamaanisha michoro miwili au herufi tatu zinazotambulisha mashirika ya usafiri wa anga.

 “Wakala Aliyeidhinishwa” inamaanisha wakala wa mauzo aliyeteuliwa nasi ili atuwakilishe katika utoaji wa huduma zetu za uchukuzi wa anga.

“Mzigo” inamaanisha mali yako binafsi unayokuwa nayo wakati wa safari. Isipokuwa kama ikibainishwa vinginevyo, inahusisha mzigo wa mkononi na wa kushikilia.

 “Risiti ya Mzigo” inamaanisha zile sehemu za tiketi, ambazo zinanahusiana na uchukuzi wa mizigo yako.

 “Kibandiko cha Utambulisho wa Mzigo” ina maanisha nyaraka inayotolewa kwa ajili ya utambulisho wa mizigo ya kushikilia.

 “Mzigo wa Kushikilia” inamaananisha mzigo ulio chini ya uangalizi wetu na ambao tumeutolea Risiti ya Mzigo.

Kikomo cha Ukaguzi” inamaanisha kikomo cha muda ulioainishwa ambao unatakiwa uwe umemaliza taratibu za ukaguzi na kupata kibali chako (Boarding pass) cha kuingia ndani ya ndege.

 “Masharti ya Mkataba” inamaanisha vifungu vilivyomo au vilivyoambatana na tiketi yako au resiti ya malipo, vikitambuliwa hivyo na vikihusisha masharti ya uchukuzi mizigo na matangazo.

 “Mkataba” inamaanisha yeyote miongoni mwa sheria zifuatazo inahusika:

Mkataba juu ya Uunganishaji wa kanuni kadhaa kuhusiana na usafirishaji wa anga kimataifa uliotiwa sahihi mjini Warsaw, tarehe 12 Octoba 1929 (hapa ukijulikana kama Mkataba wa Warsaw).

Mkataba wa Warsaw kama ulivyorekebishwa huko The Hague tarehe 28 Septemba 1955.

Mkataba wa zaiada wa Guadalajara wa mwaka 1961.

Mkataba wa Montreal wa mwaka 1999.

 “Madhara” inahusisha kifo au majeraha ya mwili kwa msafiri, upotevu wa mizigo, wizi au madhara mengine yatokanayo au yanayohusiana na uchukuzi wetu au huduma nyingine zitolewazo nasi.

 “Siku” inamaanisha siku za kalenda, ikihusisha siku saba za wiki, ikiwa kwamba, kwa lengo la tangazo, siku ambayo tangazo litatolewa haitahesabiwa; na ikiwa kwamba kwa malengo ya kuthibitisha uhalali wa tiketi, siku ambayo tiketi itatolewa, au siku ya kuanza safari, haitahesabiwa.

 “Kupuni ya Kielektroniki” ("Electronic Coupon") inamaanisha kupuni ya safari ya kielecroniki au waraka wa thamani uliopo kwenye database yetu.

 “Tiketi ya Kielekroniki” ("Electronic Ticket") inamaanisha risiti itolewayo nasi au kwa niaba yetu, kupuni za kielektroniki na, kama inahusika, waraka ya kuingia kwenye ndege.

 “Hali isiyo ya Kawaida(“Extraordinary Circumstances”) inahusisha tatizo katika uungozaji wa ndege, kuchafuka kwa hali ya hewa, taarifa juu ya tishio la usalama, ugaidi, mgomo, na mapungufu ya usalama wa ndege.

 “Silaha za Moto” ("Firearms") inamaanisha bunduki ndugondogo au salaha za mashindano.

 “Kupuni ya Safari” ("Flight Coupon") inamaanisha kipande cha tiketi chenye maandishi "good for passage, "au Kupuni ya Kielektroniki kama ni Tiketi ya Kielektroniki, na inaonyesha mwelekeo wa safari yako.

"Force Majeure" ina maanisha hali siyo ya kawaida iliyo nje ya uwezo wetu ambayo matokeo yake yasingeweza kuepukika kwa vyovyote vile.

 “Risiti” inamaanisha waraka au nyaraka zinazoonyesha jina la msafiri, taarifa za ndege na matangazo tuzitoazo kwa wasafiri wanaosafiria Tiketi za Kielektroniki.

 “Ushuru wa Forodha” ("Tariff") inamaanisha kumbukumbu za nauli, makato na /au masharti husika ya uchukuzi zilizotunzwa, inapobidi, na mamlaka husika.

 “Tiketi” inamaanisha waraka utolewao nasi au kwa niaba yetu uitwao "Passenger Ticket and Baggage Check", Tiketi ya Kielektroniki au uthibitisho wa taarifa za ndege (kiwemo namba ya uthibitisho), na unahusisha Masharti ya Mkataba, kupuni na matangazo.

 “Mzigo Usiokaguliwa” (“Unchecked Baggage”) inamaanisha Mzigo wa Kushikila ambao haujakaguliwa na kupata Kibandiko cha Utambulisho wa Mzigo.

2. KUTUMIKA

2.1 Jumla

Masharti ya Uchukuzi yaliyobainishwa hapa chini yanahusu manunuzi yote ya tiketi unayofanya kwetu na yanaainisha wajibu wetu kuhusiana na manunuzi hayo. Ndege ziendeshwazo na shirika letu kwa mfumo wa wakala anayetambulika hazihusiki na Vigezo na Masharti haya. Kila mtu wa tatu ambaye ni msambazaji unayeweza kuwa umenunua huduma au bidhaa kwake, anaweza kuwa na Vigezo na Masharti tofauti. Tafadhali hakikisha umesoma vigezo hivyo na masharti ununuapo huduma kutoka kwake.

2.1.1 Mkataba baina yako na SISI unaanza mara tu ununuapo tiketi. Hii inahusika na huduma zozote, ziwe zetu pekee au zile za msambazaji wa tatu ambaye umenunua huduma au bidhaa kwake, ambapo tulikuwa wakala aliye wazi.

2.1.2 Isipokuwa kama ilivyoelezwa katika vifungu vya 2.2, 2.4 na 2.5, Masharti yetu ya Uchukuzi yanahusika tu kwenye zile ndege, au sehemu za ndege, ambapo Number ya Utambulisho wa Shirika (Airline Designator Code ‘FN’) inaonyeshwa kwenye kisanduku cha Tiketi kwenye ndege au sehemu ya ndege hiyo. Vigezo na Masharti vilivyomo kwenye Tiketi, Risiti au waleti ya tiketi, vitakuwa sehemu ya haya Masharti ya Uchukuzi. Kama umenunua tiketi ya kuunganisha kutoka fastjet au shirika lingine, mkataba huu unakuwa tofauti. Hatudhamini au kukubali kuwajibika na kukosekana kwa ndege ya kuunganisha kwenye ndege ya fastjet inayofuata au kwenye ndege ya shirika lingine.

2.2 Ukodishaji

Kama uchukuzi unafanyika kulingana na makubaliano ya ukodishaji, Haya Masharti  ya Uchukuzi yanahusika kwa kiwango ambacho yamejumuishwa kwenye maelekezo au vinginevyo, katika makubaliano ya ukodishaji au kwenye tiketi.

2.3 Sheria Inayoongoza

Haya Masharti ya Uchukuzi yanahusika isipokuwa kama hayaendani na Tariff au sheria husika ambamo hata hizo Tariff au sheria zitatawala. Kama kipengele chochote cha Haya Masharti ya Uchukuzi kiko batili chini ya sheria husika, vipengele vingine vitaendelea kuwa halali.

2.4 Masharti kutawal Kanuni

Isipokuwa kama inavyoelezwa katika Haya Masharti ya Uchukuzi, pindi itokeapo kutorandana kati ya Masharti haya na kanuni nyingine tulizonazo, Masharti haya yatatawala.

2.5 Mabadiliko ya Masharti

Hakuna mabadiliko ya Haya Masharti ya Uchukuzi yaliyo halali isipokuwa kama yamewekwa kwenye maandishi na mmoja wa Wakurugenzi au Maafisa wetu.

2.6 Jina na anwani ya Shirika

Jina letu linaweza kufupishwa kwenye Namba yetu ya Utambulisho wa Ndege (Airline Designator Code ‘FN’), au vinginevyo, kwenye tiketi. Ofisi yetu rasmi inaonyeshwa mwishoni mwa Masharti haya. Mawasiliano yote, matangazo, n.k.,yaelekezwe kwenye anwani ya mawasiliano mwishoni mwa Masharti haya.

3. TIKETI

3.1 Vifungu vya Sheria

3.1.1 Tutatoa huduma ya uchukuzi mara uonyeshapo kumbukumbu ya tiketi yako, utambulisho wa picha unaukutambulisha kama msafiri aliyetajwa kwenye tiketi na nyaraka halisi za usafiri (k.m. Hati ya kusafiria, visa).

3.1.2 Tarehe ya kusafiri inabadirishwa baada ya malipo ya tozo husika (tazama tozo zetu na makato).

3.1.3 Gharama zote za tiketi hazirejeshwi. Unasisitiziwa kuhakikisha kuwa una bima sahihi kukugharimia pale ambapo huwezi kutumia tiketi yako.

3.1.4 Abiria wanatakiwa kuonyesha kadi walizotumia kufanya malipo sambamba na nyaraka zao za kusafiria kwa ajili ya uhakiki. Kama kadi iliyotumika kufanya malipo sio ya abiria anayesafiri, kopi za kila upande wa kadi zinatakiwa kuonyeshwa. Kopi hizo zinatakiwa ziwe zimesainiwa na mmiliki wa kadi na pia saini ifanane na ile ya kwenye kadi halisi. Abiria atakayeshindwa kuonyesha kadi iliyotumika kununulia tiketi au kopi iliyosainiwa na mmiliki hataruhusiwa kuingia kwenye ndege.

3.2 Mabadiliko ya tiketi

3.2.1 Tiketi yako ni halali kwa safari kama inavyoonyeshwa kwenye tiketi, unakotoka na mwisho wa safari kwa tarehe na namba ya ndege. Nauli uliyolipa inategemeana na Tarrif yetu na ni kwa ajili ya safari iliyoonyeshwa kwenye tiketi na inaunda kipengele muhimu cha mkataba wetu na wewe.

3.2.2 Endapo unapendelea kubadilisha tarehe ya kusafiri, unapaswa kutujulisha mapema. Gharama zozote za nyongeza (zikikokotolewa kulingana na sheria na kanuni zetu) zitakokotolewa na utapewa fursa ya kukubali bei mpya au kuendelea na usafiri wa awali kama ilivyo kwenye tiketi. Mabadiliko yote yafanyike wakati wa saa za kazi angalau masaa sita kabla ya ukaguzi na yanaweza kufanywa na msafiri aliyetajwa kwenye tiketi na/au mtu aliyenunua tiketi ya mwanzo. Tozo la dola za kimarekani 25 au kiwango sawa katika sarafu ya ndani litatozwa kwa kila badiliko la tarehe ya kusafiri.

3.2.3 Kama unataka kubadilisha tiketi yako, hivi Vigezo na Masharti vinahusika kwenye ndege tu na pale ambapo umetengeneza kumbukumbu ya safari. Kama umenunua bidhaa au huduma ya ziada kutoka kwetu tukiwa kama wakala aliyeidhinishwa na mtu wa tatu, Vigezo na Masharti ya mtu wa tatu vitahusika pamoja na haya Masharti ya Uchikuzi.

3.2.4 Kama umenunua tiketi ya ziada au tiketi ya kuunganisha, masharti ya tiketi ya mtu wa tatu yanahusika. Fastjet haikubali kuwajibika kwenye kutokuunganishwa kutokanako na mabadiliko ya ndege.

4. NAULI, KODI, ADA NA MAKATO

4.1 Nauli

Nauli zinahusika tu kutoka uwanja wa ndege wa mwanzo wa safari hadi kwenye uwanja wa ndege wa mwisho wa safari, isipokuwa kama ikielezwa vingine. Nauli hazihusishi usafiri wa aridhini baina ya viwanja vya ndge au baina ya viwanja vya ndege na miji. Nauli yako itakokotolewa kulingana na “Tarrif” yetu siku ya malipo ya tiketi.

4.2 Kodi

Kodi zinazohusika, zikipangwa na serikali au mamlaka nyingine, au na mwendeshaji wa uwanja wa ndege, zitalipwa na wewe. Wakati unaponunua tiketi, utataarifiwa kuhusiana na kodi ambazo hazijajumuishwa kwenye nauli, nyingi zake zitakuwa zimeonyeshwa tofauti kwenye tiketi. Kodi zilizopangwa kwenye usafiri wa anga zinaenda zikibadilika. Zinaweza kupangwa baada ya tarehe ya kuchukua tiketi. Kama kuna ongezeko la kodi, ada au makato lililoonyeshwa kwenye tiketi, utatakiwa kulilipa. Kadhalika, kama kodi mpya, ada, au makato vitapangwa baada ya tiketi kutolewa,  utatakiwa kuilipa. Vilevile, pale ambapo kodi, ada au makato ulivyolipia wakati tunakupa tiketi vimeondolewa au kushuka kiasi kwamba havikuhusu na kuna kiasi cha pesa kinachobaki, utakuwa na haki ya kudai kurejeshewa. Endapo hutatumia tiketi yako utakuwa na haki ya kudai kurejeshewa kodi za serikali, ukiondoa gharama za uendeshaji za dola kumi za kimarekani au kiasi sawa katika sarafu ya ndani.

4.3 Sarafu

4.3.1 Nauli na kodi vinalipwa katika dola ya kimarekani au sarafu ya nchi ambapo tiketi imetolewa, isipokuwa kama nauli mpya imeonyeshwa nasi au wakala wetu aliyeidhinishwa wakati au kabla ya malipo ( kwa mfano, kwa sababu ya kutobilishika kwa sarafu ya ndani) “sarafu ya bei”. Tunaweza, kwa uamuzi wetu, kupokea malipo katika sarafu nyingine.

4.3.2 Wasafiri wanaolipia tiketi zao kwa njia ya credit au debit card kwa sarafu tofauti na sarafu ya mauzo ya fastjet watakatwa na mtoa kadi hiyo kwa sarafu yake. Fastjet haina mamlaka juu ya viwango vya kubadilisha fedha au makato mengine yoyote yanayoweza kuwekwa na mtoa kadi.

4.3.3 Unaponunua tiketi kupitia matandao wa fastjet.com unaweza kuchagua kulipa kwa kutumia sarafu iliyoko kwenye credit card pale inapotofautiana na sarafu ya mauzo ya fastjet. Huduma inaweza kusita kwa sababu mbalimbali ikwemo sarafu zisizokubalika au matengenezo.

4.4 Ada ya uendeshaji

Tunayo haki ya kutoza kiasi fulani cha ada ya uendeshaji kwa ajili ya huduma ndogo ndogo ambazo hazimo kwenye bei ya tiketi, ikiwemo maombi ya taarifa binafsi kulingana na kifungu kidogo namba 5.3 na maombi ya resiti mbili.

4.5 Makato na Ada za Kadi za Malipo

Katika mazingira fulani wateja wanaotumia credit, debit au aina nyingine za kadi za malipo wanaweza kutozwa ada na makato ya ziada yaliyowekwa na mtoa kadi. Fastjet haina mamlaka juu ya makato na ada hizi.

5. KUWEKA NAFASI YA USAFIRI

5.1 Mambo Muhimu

5.1.1 Sisi au Wakala wetu atatunza kumbukumbu zako. Tutakupa uthibitisho wa maandishi kama utakuwa umeweka nafasi kwa njia ya simu. Ikiwa ni kwa njia ya Internet uthibitisho utaonekana kwenye skrini mwishoni mwa muamala. Ni vema kuprinti namba ya muamala huu kwa ajili ya kumbukumbu kwa sababu utatakiwa kuitaja wakati wa ukaguzi wa kuingia kwenye ndege.

5.1.2 Uwekaji nafasi hautakamilika hadi utakapopokea namba ya uthibitisho nasi kupokea malipo.

5.2 Mwisho wa kukatisha tiketi

Nauli lazima ilipwe yote baada ya uthibitisho wa nafasi ya safari. Kama nauli haijalipwa kikamilifu ndani ya ‘muda mwafaka’ au kadi yako imekataliwa, tutafuta nafasi yako wakati wowote bila kuwajibika. Hakutakuwa na uhakika wa kupata fursa ya kulipa nauli ya awali.

5.3 Muda mwafaka wa malipo

Nyakati zifuatazo zinachuliwa kuwa mwafaka na fastjet kwa ulipaji wa ulipaji wa nauli na kodi kikamilifu:

Masaa 48 kama unasafiri ndani ya mwezi

Masaa 24 kama unasafiri ndani ya siku 4

Masaa 6 kama unasafiri ndani ya chini ya siku 4

Saa 1 kama unasafiri ndani ya masaa 24

5.3. Taarifa binafsi

Utambue kuwa umetupatia taarifa binafisi kwa ajili ya kuweke nafasi, kununua na kutoa tiketi, kutunza mahesabu, kutoa bili na kukagua mahesabu (ikihusisha kukagua kadi za malipo); pia kwa ajili ya mambo ya kiutawala na kisheria, uchambuzi wa kitakwimu, uendelezaji na utoaji huduma, na usimamiaji ulinzi, uhamiaji, forodha na taratibu za kuingia kwenye nchi na kuziweka wazi taarifa hizo kwa mawakala wa serikali, kuhusiana na safari yako. Inawezekana pia kuwa taarifa hizo zinaweza kutumika kwa malengo ya mauzo na matangazo na kwamba zinaweza kuwekwa wzi kwa makampubuni ndani ya fastjet Airlines Limited au wabia wetu. Kwa malengo haya unaturuhusu kutunza na kutumia taarrifa hizi na kuzipeleka kwenye ofisi zetu, kwa kampuni tanzu, mawakala wetu, mawakala wa serikali, watunza taarifa, kampuni za kadi za malipo au watua huduma zilizotajwa hapo juu. Hii inaweza kuhusisha utumaji wa taarifa zako nje ya nchi yako. Kama hupendi kupata habari kutoka kwa kwetu au kwa wabia wetu tafadhali tuandikie kupitia anwani ya mawasiliano iliyopo baada ya Masharti ya Uchukuzi.

5.4. Mpangilio wa Siti

Abiria wanaweza kulipa gharama za ziada mapema,kujua siti yako  wakati wa kukata tiketi kabisa.uchaguzi wa siti ni pendekezo lako kama utakua hukuchagua siti utapewa kwenye kaunta la ukaguzi bila malipo.

5.4.1. Gharama za kuchagua siti

Aina mbili za pendekezo la uchaguzi wa siti zilizowekwa katika orodha ya bei na gharama.

Endapo siti itakuwa inashughuli maalum, usalama au ulinzi, tutafanya juhudi kuiheshimu siti iliyolipiwa.

5.4.2. Gharama za marejesho ya hela kwa siti zilizotengwa

Ada ya siti zilizotengwa hazirudishwi labda itokee tofauti na ibara ya 5.4.2.3

5.4.2.1.  Endapo itatokea umefuta, umechelewa au umesogeza ndege, hela ya siti yako uliyolipia kwenye ndege ya awali haitarudishwa.

5.4.2.2. Kama tutafanya mabadiliko kwenye siti uliyochagua kwa sababu hujatimiza matakwa au vigezo vilivyowekwa.

5.4.2.3. Kama itatokea tumefuta ndege yako ambayo ulichagua siti, utakuwa na haki ya kurudhishiwa hela yako ya siti au kukuhamisha kwenye siti ya karibu uliyolipia kwa njia ya simu.

5.4.3. Masharti ya Siti Zilizotengwa

5.4.3.1 Tuna haki zote kuzitumia siti zilizotengwa kwa shughuli zetu, usalama na ulinzi muda wowote wakati wa safari.

5.4.3.2 Kwa sababu za kiusalama na ulinzi, unaweza tu kukaa kwenye siti ya dharura (mtari 1 na 11) endapo:

a. Una umri wa miaka 16 au Zaidi.

b. Upo tayari na una nguvu za kumsaidia mfanyakazi ndani ya ndege endapo itatokea dharura.

c. Hausafiri na mtoto mchanga au mtoto mwenye umri chini ya miaka 16.

d. Hauhitaji mkanda wa ziada.

e. Hautahitaji msaada wa aina yoyote.

f. Hauna matatizo ya macho

5.4.4. Siti zinazopangwa uwanja wa ndege

Kwa siti zitazopangwa uwanja wa ndege na hazijanunuliwa, hatukuhakikishii siti yoyote. Tuna haki ya kukupangia na kukuhamisha siti wakati wowote, hata baada ya kuingia ndani ya ndege. Hii inaweza kuwa muhimu kwa sababu ya shughuli zetu, usalama na ulinzi.

6. SAFARI ZA KUUNGANISHA

Ndege za fastjet hazilengi kutumika kuunganisha na ndege za mashirika mengine au za fastjet. Safari yoyote ya kuunga inafanyika kwa tahadhari yako binafsi na utatakiwa kugaguliwa na mzigo wako kwenye kila ndege ya kuunganisha.

7. UKAGUZI NA KUINGIA NDEGE

7.1 Mwisho wa muda wa ukaguzi ni dakika 40 kabla ya muda uliopangwa kwa ndege kuondoka. Dawati la ukaguzi litafungwa kwa muda huo; kwa hiyo unatakiwa kujiwekea muda wa kutosha ili uweze kukaguliwa kabla ya muda huo. Hatutakuruhusu kusafiri na tutafuta tiketi yako iwapo hutafuata muda wa ukaguzi au ukionekana kutokuwa na nyaraka kamili na hauko tayari kusafiri. Hatuhusiki na upotevu wowote kutokana na kutozingatia masharti.

7.2 Unatakiwa uwe kwenye mlango wa kuingilia kwenye ndege kabla ya muda tuliokupangia wakati unakaguliwa.

7.3 Tutafuta nafasi yako endapo utashindwa kufika kwenye mlango wa kuingilia kwenye ndege kwa wakati.

7.4 Hatutawajibika kwako kuhusiana na upotevu au gharama zozote utakazoingia kutokana na kutozingatia Sheria hii.

7.5 Mlango wa kuingilia kwenye ndege utafungwa dakika 10 kabla ya muda wa kuondoka uliopangwa.

7.6 Baada ya muda huu masharti yaliyobainishwa katika vifungu namba 7.2 hadi 7.4 vitatumika.

8. KUKATAA NA UKOMO WA MIZIGO

8.1 Haki ya kukataa mzigo

Tunaweza, kwa uamzi wetu, kukataa kubeba mzigo wako endapo tumekujulisha kwa maandishi kwamba baada ya notisi ile hatutabeba tena kwenye ndege zetu. Kwa hali hii utakuwa na haki ya kurejeshewa fedha zako. Tunaweza pia kukataa kukubeba wewe au mzigo wako endapo moja au zaidi ya yafuatayo yametokea au tunaamini yanaweza tokea.

8.1.1 Uamuzi huo ni muhimu ili kutekeleza sheria, kanuni, au maagizo ya serikali.

8.1.2 Kukubeba wewe au mzigo wako kunaweza kuhatarisha usalama wa ndege au utulivu wa wasafiri wengine au wafanyakazi wa ndege.

8.1.3 Akili yako au hali ya mwili, ikihusisha matatizo yako yatokanayo na pombe au madawa, ni hatarishi kwako mwenyewe, wasafiri wengine, wafanyakazi wa ndege, au mali.

8.1.4 Umevunja sheria kwenye safari iliyopita na tunaamimi kuwa tukio hilo linaweza kujirudia.

8.1.5 Umekataa kukaguliwa

8.1.6 Hujalipa nauli, kodi, ada au makato husika.

8.1.7 Unaonekana kutokuwa na nyaraka halali za kusafiria, unaweza kutaka kuingia kwenye nchi ambayo unaunganishia safari, au ambayo huna nyaraka halali za kuingia, unaweza kuharibu nyaraka zako za kusafaria kwenye ndege, unaweza kukataa kukabidhi nyaraka zako za kusafiria kwa wafanyakazi wa ndege inapohitajika au kutukatalia kutoa nakala ya nyaraka zako za kusafiria.

8.1.8 Umeonyesha tiketi iliyopatikana kiharamu ambayo imenunuliwa kutoka kwa mtu tofauti nasi au wakala wetu, au imeripotiwa kupotea au kuibiwa, imeghushiwa, au huwezi kuthibitisha kuwa wewe ndo mwenye jina lililoko kwenye tiketi.

8.1.9 Unakataa kufuata maelekezo yetu kuhusiana na usalama na ulinzi.

8.1.10 Umetumia maneno ya vitisho kashifa au matusi kwa wafanyakazi wetu wa chini au wa ndege.

8.1.11 Kwa makusudi umeingilia utendajikazi wa mfanyakazi wa ndege.

8.1.12 Umefanya mzaha kuhusiana na tishio la bumu, silaha za kibaiolojia au kekemikali.

8.1.13 Umehatarisha usalama wa ndege au mtu yeyote ndani yake.

8.1.14 Umefanya kosa la jinai wakati wa ukaguzi au kuingia kwenye ndege au ndani ya ndege.

8.2 Msaada Maalumu

8.2.1 Ulemavu, Madawa au Afya

8.2.1.1 Kukubali kusafirisha watu walemavu, wagonjwa au watu wengine wenye kuhitaji msaada maalumu, kunategemea makubaliano yetu kabla ya safari. Taarifa zaidi zinapatikana kwenye kanuni na sheria zilizopo kwenye mtandao wetu au kwa kuomba. Wasafiri wenye ulemavu ambao wametutaarifu juu ya mahitaji yeyote maalumu wakati wa kukata tiketi na kukubaliwa, hawatakataliwa kusafiri kwa sababu ya ulemavu au mahitaji hayo maalumu.

8.2.1.2 Viti vya magurudumu vitatolewa bure. Idadi ya wasafiri wenye kuhitaji viti vya magurudumu inaweza kuwekewa kikomo kwa nyakati tofauti. Taarifa zaidi zinapatikana kwenye kanuni na sheria zilizopo kwenye mtandao wetu au kwa kuomba.

8.2.1.3 Wasafiri waliovunjika viungo, wanaoumwa au kuumia au kuugua ugonjwa sugu, watahitaji kuwa na cheti kutoka kwa daktari wao, kikithibitisha kuwa wanaweza kusafiri. Wasafiri hawataruhusiwa kusafiri bila nyaraka sahihi.

8.2.1.4 Wasafiri wanaosafiri na madawa au vimiminika vya kutumia kwenye sindano watalazimika kuwa na nyaraka husika, kama vile maelekezo ya daktari, taarifa juu ya dawa husika na matumizi yaliyokusudiwa.

8.2.2 Watoto

8.2.2.1 fastjet haipokei watoto wenye umri chini ya miaka 12. Watoto wenye umri chini ya miaka 12 lazima waambatane na mtu mwenye miaka 16 na kuendelea ambaye atawajibika kwa ajili ya mtoto.

8.2.2.2 Watoto wenye miaka 18 wanaosafiri bila wazazi au walezi wao lazima wawe na vitambulisho na fomu ya ruhusa ikiwaruhusu kusafiri bila wazazi au walezi wao.

8.2.2.3 Watoto wenye miaka 18 wanaosafiri bila wazazi au walezi wao lazima wawe na vitambulisho na fomu ya ruhusa ikiwaruhusu kusafiri bila wazazi au walezi wao.Fomu hiyo lazima ichukuliwe kutoka kituo cha polisi na ionyeshwe pamoja na kitambulisho kwenye dawati la ukaguzi na udhibiti wa pasipoti. Fomu hiyo inahitajika kwa ajili ya usafiri wa ndani na wa nje. Bila kuwa na fomu hiyo maofisa wa kudhibiti pasipoti watawazuia watoo hao kusafiri. Watoto wanaosafiri na pasipoti halali hawahitaji fomu hiyo kwani pasipoti inakuwa kama ruhusa ya wazazi. Kitabu cha Familia (Livret de Famille) siyo kitambulisho tosha cha mtoto kusafiria safari za kimataifa. Watoto wanaosafiri safari za kimataifa za fastjet lazima wawe na vitambulisho au pasipoti halisi au nyaraka nyingine muhimu.

8.2.2.4  Idadi ya watoto wenye umri chini ya miaka miwili wanaoruhusiwa kwa mtu mzima mmoja ni wawili tu.

8.2.2.5 Watoto wagonjwa au wanaoumwa ugonjwa sugu watahitaji cheti cha daktari kikithibitisha kuwa wanaweza kusafiri. Watoto wagonjwa hawataruhusiwa kusafri bila nyaraka sahihi.

8.2.3 Mama wajawazito

8.2.3.1.Akinamama wajawazito wanaweza kusafiri kwenda na kurudi hadi wiki ya 35 ya ujauzito. Kama unatarajia mapacha safari zoto inabidi zikomee wiki ya 32. Tunapendekeza kuwa ufanye mashauriano na daktari wako kabla ya kusafiri nasi. Fastjet haitawajibika kwa msukosuko wowote utakaotokana na abiria mjamzito.

8.2.3.2 Mama wajawazito ambao wako zaidi ya wiki ya 28 watahitaji cheti cha daktari kikithibitisha kuwa wanaweza kusafiri. Cheti kilichotolewa na mkunga wako hakitakubalika. Mama wajawazito hawatapokelewa kwenye ndege bila kuwa na nyaraka sahhihi.

9. MZIGO

9.1 Kiwango cha mizigo kilichoruhusiwa

9.1.1 Kitu chochote kikubwa zaidi ya mzigo wa mkononi (56 x 45 x 25cm) kitachukuliwa kama mzigo wa kushikilia.

9.1.2 ‘Mzigo wa kushikilia’ ni kitu chochote kilichopokelewa kwa kusafirishwa kwenye ndege, ikihusisha masanduku, baby buggies, rucksacks, mahema, viti vya magurudumu, scooters na walking frames. Vifaa vikubwa vya michezo, mizigo iliyozidi ukubwa, infant travel cots, viti vya magari and vifaa vya mziki vitatozwa makato tofauti.

9.1.3 Gharama za mzigo zitalipwa kulingana na mzigo uliobeba.Begi la mtoto,kiti cha kusukuma,fimbo za kutembelea zitabebwa bure. Gharama ya mzigo inategemea na uzito wa mzigo ulionunuliwa kuanzia Dola 6 kwa kilo 20 uzito wa kawaida kwa mzigo kwa safari ya kwenda tu kama italipwa kabla ya siku ya kuondoka na Dola 25 kama italipiwa uwanja wa ndege siku ya safari. Ongezeko la mzigo unaweza kulipia kwa Dola 6 kwa kilo 1 kwa safari za ndani na pia inaweza kulipiwa kwa Dola 15 kabla ya siku ya safari na Dola 30 kama utalipa uwanja wa ndege siku ya safari.Hautarudishiwa gharama wala punguzo kama begi lako nichini yak kilo 20.

9.1.4 Kama utahitaji zaidi ya kilo 20 utalipia Dola 6 kwa kila kilo. Kuna kiwango cha juu cha uzito kwa begi kisichozidi kilo 32, kutokana na sharia za afya na usalama,na hakuna abiria atakaye ruhusiwa kuwa na mzigo wa zaidi ya kilo 50.

9.1.5 Mzigo iliyolipiwa mapema gharama hazirudishwi.kama ukilipia 20kg ya mzigo na mzigo wako ukafikia kilo 18 tu, hautorudishiwa gharama ya kilo zilizopungua.

9.1.6 Mzigo mmoja kwa mtu mmoja.Hii inamaanisha sanduku moja, begi la mkononi, begi la mgongoni, la kuwekea nguo nk. Hakuna masharti ya uzito lakini uwe na uwezo wa kuviweka vizuri na kwa usalama kwenye makabati ya ndani ya ndege na upana usiozidi vipimo vya 56cm x 45cm x 25cm, yanaweza kubebwa ndani ya ndege. (Masharti yatazingatiwa tafadhari angalia maelezo chini).

9.1.7 Kwa sababu za kiafya na usalama Fasjet haiwezi kumpokea abiria  yoyote mwenye vitu vilivyozidi kilo 32 au ukubwa uzaidi 81cm (urefu),119cm (upana), and 119cm (kina). Uzito huo hautahusisha vitu vinavyotembea.

9.1.8 Mizigo isiyo na vipimo maalum na vifaa vya michezo vitalipiwa kwa gharama ya Dola 38 kwa kila mzigo kama italipiwa kwenye mtandao,kupitia watoa huduma wa fastjet au uwanjani.

9.2 Mzigo uliozidi

9.2.1 Kiwango cha uzito wa mzigo ni kilo 20 kwa mtu mmoja aliyebeba begi. Abiria walionunua tiketi pamoja na wanasafiri pamoja walio nunua tiketi,ambao kila mmoja amelipia mzigo wake hawataruhusiwa kubeba mizigo yenye uzito zaidi ya iliyolipiwa. Kama umezidisha mzigo uliobeba utalipa gharama zaidi ya Dola 6 kwa kila kilo iliyoongezeka kwa ndege zote za ndani za Fastjet na Dola 7 kwa safari za kimataifa ukiwa uwanja wa ndege.

9.2.2 kuhusu nafasi zilizopo tunaweza pia kukubali kuweka seti moja ya vifaa vya mchezo wa gofu, baiskeli moja, begi moja la vifaa vya upepo kwa kila abiria kwa gharama za Dola 38 kwa ndege. Uzito wa juu kwa vitu hivi unatakiwa kuwa chini ya kilo 20 na  isizidi kilo 32 kwa gharama ya uzito wa ziada utatumika kwa kila kilo baada ya kuzidi kilo 20. Vitu vyote vitakuwa rasmi kwa kusafirishwa na fastjet haitawajibika kuvirudisha kama kutatokea uchelewaji. Vitu vyote ambavyo havijatajwa hapo juu vitakuwa vinatakiwa kulipiwa kulingana na masharti yaliyoainishwa kwenye kipengere 9.2.1  

9.2.3 Maelezo ya gharama ya mizigo mikubwa (kubeba kwa kutumia busara zetu) inaweza kupatikana katika jedwali ya ada na gharama iliyotumwa katika mtandao wetu au zitakazopatikana kwenye maombi.

9.3 Vitu visivyokubalika kama Mizigo

9.3.1 Huruhusiwi kuweka kwenye mzigo wako vitu vifuatavyo:

9.3.1.1 vitu ambavyo vinaweza kuhatarisha ndege au watu au mali kwenye ndege, kama vile vilivyoainishwa na Shirika la Kimataifa la Usafirishaji wa Anga “the International Civil Aviation Organization (ICAO)” Technical Instructions for the Safe Transport of Dangerous Goods by Air and the International Air Transport Association (IATA) Dangerous Goods Regulations, na kwenye kanuni zetu ( taarifa zaidi zinapatikana toka kwetu).

9.3.1.2 vitu ambavyo usafirishaji wake umezuiliwa na sheria, kanuni au maagizo ya nchi husika kuwa visitolewe au kuingizwa nchini.

9.3.1.3 vitu ambavyo tunavichukulia kuwa havistahili kusafirishwa kwa sababu ni hatarishi, si salama au kutokana na uzito, ukubwa umbo au aina, au ambavyo viko teketeke au huharibika upesi (angalia sehemu 9.12) kuhusiana na, pamoja na vitu vingine, aina ya ndege inayotumika. (Habari kuhusu mizigo isiyokubalika inapatikana kwa kuomba).

9.3.2 Visu vya nyumbani na vitu kama hivyo vinaweza kukubaliwa kama mizigo ya kushikilia, kwa uamzi wetu, lakini havitaruhusiwa ndani ya ndege. Vinatakiwa vikabidhiwe wakati wa ukaguzi.

9.3.3 Usiweke hela, vito, dhima au vitu vya thamani, nyaraka za biashara, hati za kusafiria na vitu vingine vya utambulisho.

9.3.4 Endapo, licha ya kuwa imezuiliwa, vitu vyovyote vilivyoongelewa kwenye sehemu 9.3.1, 9.3.2 na 9.3.4 hapo juu vitawekwa kwenye mzigo wako, hatutawajibika na upotevu au uharibifu wa vitu hivyo.

9.4 Haki ya kukataa kubeba mzigo

9.4.1 Kulingana na aya ya 9.3.2 na 9.3.3, tutakataa kubeba mama mzigo vitu vilivyotajwa sehemu 9.3, na tunaweza kukataa ubebaji mwingine wa vitu kama hivyo tunapovibaini.

9.4.2 Tunaweza kukataa kubeba kama mzigo kitu chochote ambacho tunaamini kuwa hakistahili kusafirishwa kutokana na ukubwa, umbo, uzito, vilivyomo ndani, aina, au usalama au sababu za kiuendeshaji, au utulivu wa wasafiri. (Habari kuhusu mizigo isiyokubalika inapatikana kwa kuomba).

9.4.3 Tunaweza kukataa kupokea mzigo isipokuwa kama umefungwa vema kwenye vyombo vinavyostahili. Habari kuhusu upakiaji unaokubalika zinapatikana kutoka kwetu kwa kuomba.

9.5 Haki ya Upekuzi

Kwa sababu za kiulinzi na kiusalama tunaweza kukuomba uruhusu kupekuliwa na kupigwa scan wewe mwenyewe na mzigo wako. Kama haupo mzigo wako unaweza kupekeuliwa kubaini kama umebeba au begi lako lina kitu chochote kati ya vilivyotajwa sehemu 9.31 au silaha au zana yoyote ya moto, risasi, ambavyo havijakabidhiwa kwetu kulingana na sehemu 9.3.2 au 9.3.3. Kama hauko tayari kukubaliana na ombi hilo, tunaweza kukataa kukubeba na mzigo wako. Pale upekuzi kwa scan unapoharibu mzigo wako, hatutawajibika isipokuwa kama ni makosa au uzembe wetu.

9.6 Mzigo wa Kushikilia

9.6.1 Ukitukabidhi mzigo wako ambao unataka ukaguliwe tutauhifadhi na kukupatia Kibandiko cha Utambulisho wa Mzigo “Baggage Identification Tag” kwa kila mzigo.

9.6.2 Mzigo wa Kushikilia lazima ubandikwe jina lako au taarifa nyinginezo za utambulisho.

9.6.3 Pale inapowezekana, Mzigo wa Kushikilia utasafirishwa kwenye ndege utakayopanda, isipokuwa kama tunaamua kuusafirisha kwenye ndege inayofuata kwa sababu za kiulinzi, kiusalama au kiuendeshaji. Kama mzigo wako utasafirishwa kwenye ndege inayofuata, tutaufikisha kwako, isipokuwa kama sheria husika inakutaka uwepo kwa ajili ya maswala ya forodha.

9.7 Mzigo wa Mkononi

9.7.1 Unaruhusiwa kubeba mzigo mmoja wa mkunoni wenye vipimo (56 cm x 45 cm x 25 cm) bila ukomo wa uzito, ingawa lazima uweze kuupakia na kuweka vema kwenye sehemu ya mizigo juu ya kichwa. Kama begi lako limezidi vipimo hivi au uzito, au linaonekana si salama, lazima lisafirishwe kama mzigo wa kushikilia aidha kwa malipo uliyolipa au kwa makato zaidi kulingana na sehemu 9.2.1.

9.7.2 Wakati wa ukaguzi begi lililo ruhusiwa litawekwa kibandiko cha utambulisho. Mizigo migine itakaguliwa kama mizigo ya kushikiliwa. Mzigo wa mkononi wa ziada utakaogunduliwa uwanjani utatozwa dola 15 au kiasi sawa kwenye sarafu ya ndani kulingana na sehemu 9.1.3.

9.7.3 Vitu visivyostahili kubebwa ndani ya sehemu ya mizigo ( kama vili vifaa teketeke vya mziki), na ambavyo havikidhi matakwa ya sehemu ya 9.7.1 hapo juu, vitakubaliwa kubebwa ndani ya ndege kama umetoa taarifa mapema na kukubaliwa. Unaweza kutakiwa kulipa makato tofauti kwa huduma hii.

9.8 Kuchukua na Kusambaza Mizigo ya Kushikilia

9.8.1 Kulingana na kifungu namba 9.6.3, unatakiwa kuchukua mzigo wako mara tu unapofikishwa mwisho wa safari yako. Ukichelewa kuuchukua kwa muda mwafaka, tunaweza kukutoza ada ya kuutunza. Kama mzigo wako hautadaiwa kwa muda wa mwezi mmoja tangu ufikishwe, tunaweza kuutupa bila kuwajibika kwako.

9.8.2 Ni yule tu mwenye Baggage Check na Baggage Identification Tag anayeruhusiwa kupelekewa mzigo.

9.8.3 Iwapo mtu anayedai mzigo hana vithibitisho, tutampatia mzigo kwa masharti kwamba anatudhibitishia kikamilifu uhalali wake.

9.9 Wanyama

9.9.1 Hatutapokea wanyama waliokufa au wazima kwenye ndege au kwenye sehemu ya mizigo isipokuwa sehemu ya 9.9.2 kwa safari zilizothibitishwa.

9.9.2 Usafirishaji wa samaki kwenda sokoni (waliokufa na wasiokuwa kwenye maji ya bahari) unaruhusiwa kwa ada na makato sahihi. Vyombo vya kusafirishia samaki lazima vifungwe kimadhubuti kuzuia kuvuja au kutoa harufu.

9.10 Mabaki ya binadamu: Jeneza, au majivu ya maiti iliyochomwa

Fastjet inapokea mabaki ya mwili (maiti) ikiwa kwenye jeneza kwa kusafirishwa katika miji ya hapahapa Tanzania ambako fastjet inafika. Mpango huo wa kubeba maiti au mabaki unatakiwa kuzungumzwa na kupangwa na kampuni ya BidAir inayofanya kazi za ubebaji wa mizigo na fastjet pamoja na wanaohusika na msiba.

Kupakia majivu ya mwili wa marehemu pia inaruhusiwa: japokuwa nakala ya cheti cha kifo na hati ya kuchoma maiti lazima viambatinishwe. Abiria anayemiliki majivu ni lazima ahakikishe kuwa yamefungwa salama katika chombo kinachofaa na pia ni lazima awe na majivu mengine kwenye begi lake la mkononi. Pia tunashauri kwamba wakala wa ubebaji ni lazima apewe taarifa wakati wa ukaguzi. Ubebaji wa viungo vingine vya binadamu hauruhusiwi. 

9.11 Silaha za moto

Silaha za mkononi zinasafirishwa tu kwenye safari za ndani ya Tanzania.

Bunduki za michezo au mashindano zinasafirishwa kwa dola 20 kila moja kwa safari moja, kulingana na masharti yafuatayo kuhusu safari za ndani ya Tanzania na safari kati ya Tanzannia na Afrika Kusini.

9.11.1 Wasafiri wenye umri zaidi ya miaka 18 lazima waonyeshe nyaraka halisi kuthibitisha uhali wa umiliki wa silaha hizo. Bila nyaraka hizo hakuna silaha itakayosafirishwa.

9.11.2 Silaha za moto zinasimamiwa na taratibu za kiusalama, hivyo inapendekezwa kukaguliwa masaa mawili kabla ya safari.

9.11.3 Bunduki lazima zibebwe kwenye masanduku magumu yanayofungika.

9.11.4 Risasi za uzito wa kilo tano zinaweza kubebwa pia, kama zitapakiwa tofauti kwenye mzigo mwingine wa kushikilia.

9.12 Bidhaa mbichi na zinazoharibika

Usafirishaji wa hadi kilo 20 za bidhaa zinazoharibika upesi kama vile matunda, mbogamboga au maua unaruhusiwa kwenye safari za ndani ya Tanzania tu kama sehemu ya mzigo wa kushikilia kwa gharama stahiki. Bidhaa ziharibikazo hazitasafirishwa kama zitakuwa zimepuliziwa dawa za kuua wadudu.

10. RATIBA, KUCHELEWA NA KUFUTWA KWA SAFARI

10.1 Ratiba

10.1.1 Muda ulioonyeshwa kwenye mtandao wa fastjet, kwenye vituo vyetu vya huduma kwa wateja au kwa wakala wetu unaweza kubadilika. Hatutoi uhakika wa muda wa safari na siyo sehemu ya mkataba wetu na wewe.

10.1.2 Kabla hatujakuuzia tiketi tutakupa ratiba ya safari kwa wakati huu, na itaonyeshwa kwenye tiketi yako. Inawezekana tukahitajika kubadilisha muda wa safari na kama ukitupatia taarifa zako zamawasiliano, tutajitahidi kukujulisha kuhusu mabadiliko hayo. Endapo, baada ya kununua tiketi yako tunafanya mabadiliko makubwa kwenye ratiba ya safari ambayo hukubaliani nayo, na hatuna uwezo wa kukuandalia safari kwenye ndege nyingine ambayo unakubaliana nayo, utakuwa na haki ya kurejeshewa fadha zako kulingana na kifungu namba.

10.2 Kufuta, Kubadilisha, kuchelewesha safari, n.k.

10.2.1 Tutafanya kila njia kuhakikisha kuwa hatukucheleweshi wewe na mzigo wako na kuzuia kufutwa ka safari.

10.2.2 Isipokuwa kama ikielezwa tofauti na Mkataba, kama tukifuta safari, tukishindwa kusafiri kulingana na ratiba au, tukishindwa kutua kwenye kituo chako, tutafanya kwa upendeleo wako ama:

10.2.2.1 kusafirisha mapema zaidi iwezekanavyo au inapowezekana, tutarefusha uhalali wa tiketi yako; au

10.2.2.4 kurejeshea fedha zako kulingana na kifungu namba 11.2.

10.2.3 Pale lolote kati ya matukio yaliyotajwa kwenye kifungu namba 10.2.2, isipokuwa kama itaelezwa vingine na Mkataba, ufumbuzi ulioainishwa kwenye kifungu namba 10.2.2 hadi 10.2.2.1 utakuwa ndo njia pekee ya utatuzi wa tatizo na hatutawajibika kwako tena.

10.2.4 Endapo kutakuwa na kufutwa kwa safari fastjet haitakufidia zaidi ya kukurejea nauli yako. Madai hay ya marejesho yanaweza kufanywa kupitia anwani ilitolewa baada haya ya Masharti ya Uchukuzi.

10.2.5 Kama safari yako itafutwa kutokana na Mazingira Yasiyo ya Kawaida ambayo kwa vyovyote vile yasingeweza kuzuilika, hutakuwa na haki ya kufidiwa zaidi ya kuwa na haki ya kufuta safari na kudai kurejeshewa nauli au kununua tiketi upya bila makato.

10.2.6 Fastjet haina uhusiana wowote na mashirika mengine. Kwa hiyo, fastjet haiwezi kuwajibika kwa ajili ya kuchelewa kupanda ndege ya kuunganisha kutokana na kuchelwa au kupishana kwa ratiba ya safari kwenye aidha ndege nyingine ya fastjet au shirika lingine.

11. KURUDISHWA KWA FEDHA

11.1 Kulingana na vigezo vilivyomo humu, nauli zote hazirejeshwi. Tiketi zinaweza kubadilishwa kwenda safari nyingine kwa bei ileile au ya juu kidogo kulingana na uwepo wa nafasi, malipo ya ada ya kubadilisha na tofauti yoyote katika nauli. Taarifa kamili zinaweza patikana kwenye kifungu chetu cha ada na makato. Tafadhali angalia kanuni za nauli kabla ya kukata tiketi.

11.2 Iwapo tutashindwa kutoa usafiri kulingana na mkataba, tutafanya marejesho ya nauli au sehemu yake kulingana na sheria hii.

11.2.1 Tutawajibika kumrejeshea nauli ama mtu aliyetajwa kwenye tiketi au yule aliyelipia tiketi baada ya kutoa vielelezo sahihi vya ulipaji.

11.3 Marejesho yasiyo ya hiari

11.3.1 Kama tukifuta safari au tukashindwa kusimama kwenye kituo chako na kukiwa hakuna ndege mbadala, au kama marejesho hayo ni halali yako kulingana na haya Masharti ya Uchukuzi, kiasi cha marejesho kitakuwa:

11.3.1.1 kiasi cha nauli iliyolipwa, kama hakuna sehemu ya tiketi ambayo imeshatumika.

11.3.1.2 kama sehemu ya tiketi imeshatumika, marejesho yatakuwa ile tofauti kati ya nauli iliyolipwa na nauli nauli iliyotumika.

11.3.2  Kulingana na kifungu cha 14, hatutawajibika kwa gharama yoyote utakayoingia kuhusiana na kufutwa kwa safari au kukosa kupitiliza kituo. Unashauriwa kukata bima ya kutosha kwa ajili ya safari yako.

11.3.3 Maombi ya marejesho ya nauli yafanyike kwa maandishi kupitia anwani iliyowekwa baada ya haya Masharti ya uchukuzi.

11.4 Sarafu

Tunayo haki ya kurejesha nauli kwa sarafu sawa na iliyotumika wakati wa kununua tiketi.

12. TABIA NDANI YA NDEGE

12.1.1 Iwapo, kwa maoni yetu, ukionyesha tabia ndani ya ndege ambazo ni hatarishi kwa ndege au mtu yeyote au mali, au zinazuia wafanyakazi kutekeleza majukumu yao, au unashindwa kufuata maelekezo ya wafanyakazi ndani ya ndge yakiwemo ya uvutaji wa sigara, ulevi au utumiaji wa madawa ya kulevya, au zinavuruga amani, zinaharibu au kujeruhi wasafiri wengine au wafanyakazi wa ndege, tunaweza kuchukua hatua zozote kadili tunavyoona zinafaa kuuzuia mwendelezo wa tabia hiyo. Unaweza kushushwa na kukataliwa kuunganisha safari kwenye uwanja wowote, na unaweza kushtakiwa kwa makosa uliyotenda.

12.1.2 Endapo, kutokana na tabia zako tunalazimika kutua kwenye uwanja ambao si mwelekeo wetu na tukakushusha, utalazimika kutulipa gharama zote za kuchepusha safari na faini zozote zitakazodaiwa na serikali ya nchi ambayo tumetua kwa dharura.

12.1.3 Ili kuondoa mashaka, hauruhusiwe kunywa vilevi ambavyo havijanunuliwa kutoka kwa wafanyakazi wetu ndani ya ndege. Vilevi visivyolipiwa ushuru (Duty Free alcohol) haviruhusiwi kunywewa ndani ya ndege na vinatakiwa visifunguliwe. Tunayo haki ya kukataa kukuuzia vilevi ndani ya ndege.

12.2 Vifaa vya Kielektroniki

Kwa sababu za kiusalama tunaweza kuzuia matumizi ya vifaa vya kielektroniki, ikihusisha simu za kiganjani, kumpyuta mpakato (Laptop computers), rekoda, radio, CD players, na electronic games. Matumizi ya vifaa vya kusikia na vya kuongoza mapigo ya moyo vinaruhusiwa.

13. SERVICESMIPANGO YA HUDUMA ZA NYONGEZA

Kama tukipanga kukupatia huduma zozote kupitia kwa  mtu yeyote wa tatu mbali na uchukuzi kwa ndege, au kama tukitoa tiketi au vocha kuhusiana na usafirishaji au huduma (mbali na uchukuzi kwa ndege) itolewayo na mtu wa tatu kama vile kuweka nafasi ya malazi hotelini au kukodisha magari, sisi tunahusika kama wakala wako tu. Vigezo na masharti ya mtoa huduma wa tatu vitatumika.

14. TARATIBU ZA UENDESHAJI

14.1 Jumla

14.1.1 Unawajibika kupata nyaraka zote za kusafiria pamoja na visa, na kufuata sheria, kanuni, maelekezo, na matakwa ya safari ya nchi unakotoka, kwenda au kupitia.

14.1.2 Hatutawajibika kwa yatakoyomtokea abiria yeyote atakayeshindwa kupata nyaraka husika kisheria au kufuata kanuni, maelekezo, matakwa, na masharti

14.2 Nyaraka za Kusafiria

Kabla ya safari lazima uonyeshe nyaraka zote husika kuhusiana na kutoka, kuingia, afya na nyinginezo zinazohitajika kisheria, kanuni, maagizo, na matakwa ya nchi husika, na uturuhusu kuchukua na kushikilia nakala zake. Tunayo haki ya kukataa kukusafirisha endapo hutakuwa umetekeleza matakwa haya, au kama nyaraka zako za safari hazitakamilika.

14.3 Kukataliwa kuingia nchini

Kama hutaruhusiwa kuingia kwenye nchi fulani, utalazimika kutulipa gharama zozote tutakazotozwa na nchi husika na gharama za kukusafirisha hadi kwenye nchi hiyo na hatutakurejeshea nauli utakayotozwa kutoka nchi hiyo.

14.4 Passenger Responsible for Fines etc Faini za Abiria

Endapo tutalazimika kulipa faini yoyote kutokana na kushindwa kwako kufuata sheria, kanuni, matakwa au mahitaji mengine yoyote ya nchi husika au ukashindwa kuonyesha nyaraka zinazotakiwa, tutakutaka uturudishie gharama hizo. Tunaweza kukata malipo hayo kutoka kwenye safari ambayo haijatumika au kwenye tiketi yako, au kwenye fedha zozote ambazo ziko mikononi mwetu.

14.5 Forodha na Ukaguzi

Kama itabidi, mizigo yako itakaguliwa na maafisa wa forodha au maafisa wengine wa serikali. Hatutawajibika kwako kuhusiana na upotevu au uharibifu wowote utakaotokea wakati wa ukaguzi huo au kutokana na kushindwa kwako kufuata matakwa haya.

14.6 Ukaguzi wa kiusalama

Utatii ukaguzi wote utakaofanywa na maafisa wa serikali, maafisa wa viwanja vya ndege, mashirika ya ndege au sisi.

14.7 Gharama za Matibabu na Michepuko

Kama utaugua ghafla ukiwa kwenye ndege na tukaamua kuwa ni vema kukushusha kwa manufaa yako ili upate huduma stahiki, utawajibika kulipa gharama zozote za matibabu pamoja na za malazi ya wanafamilia au marafiki watakaokuwa wanakuangalia na gharama za safari ya kuendelea unakokwenda. Tunapendekeza kuwa ukate bima ya kutosha kabla ya kuanza safari yako.

14.8 Machapisho

Isipokuwa pale ambapo kwa makusudi na tukijua kuwa matendo au uzembe wetu vitasababisha madhara, hatutawajibika kwa makosa kwenye ratiba au machapisho mengineyo kuhusiana na tarehe, muda wa kuondoka au kufika au uendeshaji wa ndege yoyote.

15. DHIMA YA UHARIBIFU

15.1 Dhima yetu itaamuliwa na Masharti yetu ya Uchukuzi. Dhima yetu inakikomo, hivyo unashauriwa kuchukua bima ya kutosha kwa safari yako. Vifungu vyetu kuhusu dhima ni kama ifuatavyo:

15.1.1 Isipokuwa kama ikielezwa vinginevyo humu, usafiri wa kimataifa, kama ulivyoelezwa kwenye Mkataba, unategemea kanuni za dhima za Mkataba.

15.1.2(a) Dhima yoyote tuliyonayo kuhusu uharibifu itapunguzwa na uzembe wowote toka kwako utakaosababisha au kuchangia kwenye uharibifu huo kulingana na sheria husika.

15.1.2(b) Tutawajibika tu kwa uharibifu utokeao wakati wa usafirishaji kwenye ndege au sehemu ya ndege yenye namba ya utambulisho wa ndege (Airline Designator Code 'FN' ) yetu.

15.1.2(c) Hatutawajibika kwa uharibifu wa mzigo ambao haujakaguliwa isipokuwa kama uharibifu huo utatokana na uzembe wetu.

15.1.2(d) Hatutawajibika kwa uharibifu wowote utokanao na sisi kutimiza sheria husika au sheria na kanuni za serikali, au kushindwa kwako kuzitimiza.

15.1.2(e) Isipokuwa pale ambapo kwa makusudi na tukijua kuwa matendo au uzembe wetu vitasababisha uharibifu wa mzigo wa kushikilia, dhima yetu itakomea kwenye SDR 19 (approx. $11.05) kwa kilo na kwa mzigo usiopimwa itakomea kwenye SDR 332 ($215.80) kwa abiria mmoja ambapo Mkataba wa Warsaw utatumika kwenye safari yako au 1131 SDRs ($735.15) kwa Mzigo wa Kushikilia na Usiokaguliwa “Hold and Unchecked Baggage”, ikitegemea uthibitisho wa uharibifu wa mzigo usiopimwa ambapo Mkataba wa Montreal utatumika kwenye safari yako uliyosafiri siku au baada ya tarehe 28 June 2004, ikiwa kwamba kwa kila tukio, kulingana na sheria husika, viwango tofauti vya dhima vinatumika. SDR ni Haki Maalumu ya Kubadilisha pesa “Special Drawing Right” kama ilivyoelezewa na Shrika la Fedha Duniani (IMF). Thamani ya 1 SDR inakaribia sent.za kimarekani 65 kama ilivyokuwa tarahe 1October 2012, lakini kiwango hiki kinaweza kubadilika kama inavyoonyeshwa kwenye mtandao wa IMF (imf.ofg). Kwa malengo ya Mkataba wa Warsaw “Warsaw Convention”, kama uzito wa mzigo haujaandikwa kwenye risiti ya ukaguzi, inachukuliwa kuwa uzito wa mzigo huo hauzidi ule ulioruhusiwa kama mzigo wa mkononi. Kama thamani kubwa itadaiwa kimaandishi kuhusiana na mzigo wa kushikilia kulingana, dhima yetu itakomea kwenye thamani hiyo iliyodaiwa.

15.1.2(f) Isipokuwa pale ambapo kifungu kingine mahsusi kimetajwa kwenye Masharti haya, tutawajibika kukulipa fidia ya uharibifu unaorekebishika na uliothibitishwa kulingana na Mkataba.

15.1.2(g) Hatutawajibika kwa uharibifu usababishwao na begi lako. Utawajibika kwa uharibifu wowote utakaotokana na mzigo wako kwenye begi la mtu mwingine au mali, ikiwemo mali yetu.

15.1.2(h) Hatutawajibika kwa uharibifu utakaotokea kwenye vitu ambavyo havimo kwenye mzigo wa kushikilia kulingana na kifungu cha 8.3, ikiwemo vitu teketeke au viharibikavyo haraka, vitu vya thamani, kama vile pesa, vito, madini, kompyuta, vifaa vya umeme, nyaraka za makubaliano, dhima, au vitu vingine, nyaraka za kibiashara, pasipoti, na nyaraka nyingine za utambulisho.

15.1.2(i) Hatuhusiki na ugonjwa, majereha au ulemavu, kikiwemo kifo, vinavyohusishwa na udhoofu wako wa mwili au kuzidi kwa hali hiyo.

15.1.2(j) Mkataba wa uchukuzi, ukihusisha Mkataba huu na vikomo vya dhima, unahusu mawakala, watumishi, waajiriwa, na wawakilishi wetu kwa kiasi sawa kama unavyotuhusu sisi. Kiasi cha pesa kinachotoka kwetu na mawakala, waajiri, na wawakilishi wetu, hakitazidi kiwango cha dhima yetu, kama kipo.

15.1.2(k) Hakuna kitu katika Masharti haya ya Uchukuzi kitachoondoa unafuu au ukomo wa dhima yetu chini ya mkataba huu au sheria husika isipokuwa kama ikielezwa vinginevyo.

15.1.2(l) Shirika halitawajibika kwa uharibifu au upotevu utakaotokea kutokana na sehemu za mzigo zinazochomoza kama vile matairi au begi teketeke na bovu (au madhara madogo kama vile michubuko, vumbi, madoa) ikiwa matokeo ya harakati za usafirishaji wa anga au madhara ya maji kwa mizigo isiyostahimili maji.

Makubaliano Maalumu

15.2 Kuhusiana na madai yoyote kuhusu fidia itokanayo na kifo au kujeruhiwa kwa abiria katika ajali (katika harakati za kupanda na kushuka) kwenye ndege zetu.

15.2.1 hatutafuta ukomo wa dhima kwenye kifungu 22 (1) cha Mkataba au vigezo kama hivyo vilivyopo kisheria;

15.2.2 hatutajitokeza kwa utetezi chini ya kifungu namba 20 cha Mkataba, au utetezi wowote wa aina hiyo uliopo kisheria, kuhusiana na madai yasiyozidi SDRs 113,100 (Dola 65, 000);

15.2.3 Bila kuchelewa na ndani ya siku 15 baada ya mtu anayefidiwa kutambulika, tutamlipa malipo ya awali kulingana na matatizo aliyoyapata (kiasi kile kisiwe chini ya SDR16, 000 kwa abiria (dola 10,400 kama ni kifo).

Malipo yoyote ya aina hiyo hayatakuwa na dhima na yanaweza kuondolewa kwenye malipo yetu mengine, ila yatarudishwa iwapo uharibifu utakuwa umechangiwa au kusababishwa na uzembe wa abiria au mtu aliyepokea malipo hayo, au kama mtu aliyelipwa hakuwa muhusika; ikiwa kwamba tuna haki zote za utetezi (iwe ndani ya Mkataba au vinginevyo) na tuna haki zote za kuchangia.

16. KIKOMO CHA MUDA WA MADAI

16.1 Notisi ya Madai

Kupokea mzigo bila malalamiko ni ushahidi tosha kuwa mzigo umepokelewa ukiwa katika hali nzuri kulingana na mkataba wa uchukuzi, isipokuwa kama ukithibitisha tofauti.

Kama unataka kudai kuhusu uharibifu wa mzigo wa kushikilia, ni vema kututaarifu mara tu unapogundua uharibifu. Kama unataka kudai fidia kulingana na mzigo uliochelewa tutaarifu ndani ya siku 21 tangu ulipokabidhiwa mzigo wako. Kila taarifa ya namna hiyo lazima ifanywe kwa maandishi.

16.2 Kikomo cha uchukuaji hatua

Haki yoyote ya uharibifu itafutika kama madai hayatakuja ndani ya miaka miwili baada ya tarehe ya kufika mwisho wa safari, au tarehe ambayo ndege ilitakiwa kufika, au tarehe ambayo usafirishaji ulisita. Sheria ya mahakama ambako kesi inasikilizwa itaamua jinsi ya kukokotoa muda wa dhima.

17. MASHARTI MENGINE

Usafiri wako na mzigo wako pia viko chini ya masharti na kanuni nyingine zinazotuhusu au tulizorithi. Hizi kanuni na masharti ni muhimu sana. Zinahusu, pamoja na mambo mengine, usafirishaji wa watoto wasiosindikizwa, mama wajawazito, na abiria wagonjwa. Masharti juu ya matumizi ya vifaa vya kielektroniki, na matumizi ya vilevi kwenye ndege.

Kanuni na masharti juu ya mambo haya vinapatikana kwetu kwa kuomba.

18. TAFSIRI

Maelezo ya haya Masharti ya Uchukuzi ni kwa ufanisi tu, na hayatakiwi kutumika katika kutafsiri andiko hili.

Shirika la Ndege la Fastjet

Ground Floor

 Ten West

10 Vingunguti

Nyerere Road

Dar es Salaam

Muhimu: Kumbuka kwamba bei zote ziko kwa USD; Kiwango cha kibadilisha fedha kitakachotumika kuanzia 28/08/2015 ni US$1 = TZS 2,200; ZAR 13; UGX 4,000; ZMW 8.5; MWK 600, KES 110.

28/06/2015