Beba ndoo yako ya samaki na anza safari yako na fastjet kutoka Mwanza

Amini usiamini sasa wateja wa fastjet wanaweza kubeba hadi kilo 23 za samaki fresh kama Sato, sangara, furu, dagaa wa Mwanza na kamongo wote wanaruhusiwa. Hakikisha umewagandisha kabla ya kuwasafirisha na pia hakikisha umewa weka kwenye ndoo ili. Hapa tumekuwekea sababu nyingine chache za kwanini utembelee Mwanza.

Ni sehemu nzuri ya kuangalia Mandhari ya jiji

Katika muda huu wa mwaka Mwanza ni pakavu, ni muda saqhihi wa kwenda kutembelea vivutio vya kitalii, kipindi hiki hakina fukoto la joto hivyo ni kipindi muafaka kwako. Njoo na darubini yako, vaa nguo zitakazokuweka huru na beba dawa ya mbu endapo itahitajika.

Mwanza inapakana na Ziwa Victoria

Ndo kwanza umeamka na unaingiza miguu yako ndani ya ziwa Victoria, ziwa kubwa zaidi ndani ya Bara la Afrika. Hapa unaweza kununua tiketi ya kwenda kufanya matembezi na boti, uona jua likizama, kuvua samaki na mengine mengi. Pia kuna Kisiwa cha Saa nane ambacho pia ni hifadhi ya Taifa, inachukua dakika 10 kufika hapa ukitokea mjini. Hapa utaona ndege wa aina mbalimbali, Tembo, Pundamilia, twiga na Wanyama wengine. Beba chakula chako cha mchana, tafuta sehemu nzuri chini ya mti na ufurahie mazingira.

Safiri na fastjet – Hizi ndio sababu 

Tukiwa kama kampuni yenye bei ambazo kila mtu anazimudu, tunakupa bei ambayo inakufanya uokoe pesa na kufurahia safari yako. Na kwasababu tuna ndege aina ya E190 zenye madirisha makubwa Zaidi, zinakupa uhuru Zaidi wa kuangalia nje. Usisahau kununua ndoo yako ya samaki kabla ya siku ya safari


Nunua tiketi yako kupitia kituo chetu cha huduma kwa wateja, mtandaoni, ofisi za fastjet au kwa wakala wa safari za anga aliye karibu nawe. Unaweza kulipia tiketi yako kupitia credit au Debit card,  M pesa

Safiri na fastjet na ugundue urahisi  wa kufika kwenye vituo vyako pendwa ndani ya Afrika Mashariki.