Fastjet kwenda Mbeya – Kwa mpenda matembezi, huku ndio kunakufaa

Unaweza kupanda milima, kuangalia ndege warukao angani, kwenda safari na picnic ukifurahia Ngozi Crater. Mbeya ni mji mzuri kutembelea pale unapotaka kuondokana na kelele za mjini. Kitu kizuri Zaidi ni kwamba fastjet itakupeleka Mbeya kwa muda mfupi sana. Hizi ndizo sababu za wewe kuweka Mbeya kwenye orodha ya sehemu za kutembelea.

Mbeya ni sehemu nzuri kwa wanaopenda kutembea Zaidi nje. Hii ni sehemu nzuri kwa kupanda vilima hivyo chukua buti na begi lako tayari kwa kuanza safari ya kuona uzuri wa Mbeya

Anza asubuhi yako kwa kupanda mlima Loleza wenye urefu wa mita 2650,ni lazima utatoka jasho utakapokuwa ukirejea kutoka kwenye safai hii ya nusu siku. Beba maji ya kutosha sababu kadri unavyopanda juu saa nyingine joto huongezeka hivyo maji ni muhimu. Paka mafuta ya kuzuia jua kuharibu Ngozi, hasa kama ni mzungu.

Kama miguu yako itakuwa imechoka sana andaa gari kukupeleka hifadhi ya Taifa ya kitulo mchana huo. Nenda kajionee vilima vizuri vyenye maua ya kupendeza, maporomoko ya maji na vipepeo. Ni sehemu nzuri ya kufanya Yoga. Kam unataka kujifunza kuhusu uoto wa asili, Japhari Ngogo ambaye ni muongoza watalii atakusaidia.

Usiache kwenda kuona Kimondo cha Mbozi, moja ya vimondo vikubwa Duniani. Wanajografia naamini watafurahia kukiona.

Andaa safari yako na Gazelle Safaris. Muongoza safari anatembea na encyclopaedia, ambayo ina habari zote nzuri za sehemu husika. Waongoza safari hawa wanajua sehemu kila kitu kinapatikama. Njoo na Camera yako na usiogope kuuliza maswali

Baada ya kupumzika sasa nyanyuka na nenda Ngozi crater. Sehemu hii ni nzuri kama peponi ya duniani. Msituu huu uliojaa sauti nzuri za vindege itafanya safari yako kuwa nzuri zaidi.

Baada ya wiki endi kuisha  safari na ndege ya fastjet kurudi nyumbani. Wahudumu wetu wetu watakuhudumia vizuri sana na utafurahia likizo yako.

Kwa bei bomba, safari na fastjet – Kampuni ya ndege kwa wote