Fastjet yafanikisha tena rekodi mpya ya kutua na kuondoka kwa wakati ndani ya Tanzania kwa mwezi Februari

FOR IMMEDIATE RELEASE

8-03-2018

Dar es salaam: Shirika la ndege la bei nafuu Fastjet limefanikisha tena rekodi mpya ya 94% ya kutua na kuondoka kwa wakati ndani ya Tanzania kwa mwezi Fenbruari; Hii inafuatia Matokeo mazuri ambayo shirika hili lilipata mwezi Januari ambapo shirika lilipata rekodi ya 91% ya kufika na kuondoka kwa wakati. Kwenye nchi zote ambazo Fastjet inafanya shughuli zake , Shirika limeweza kuwa na 93% ya kuondoka na kufika kwa wakati. Kwa ujumla Fastjet imeruka zaidi ya safari 900 kwa mwezi Februari.

“Urahisi wa upatikanaji wa tiketi zetu ni moja wapo ya huduma bora kwa wateja kwenye shirika” Alisema msemaji wa Fastjet Tanzania Lucy Mbogoro. “Fastjet imeendelea kuboresha biashara na kuwa na nia moja ya kuhakikisha inawaletea watanzania usafiri wa bei nafuu na wakuaminika” Fastjet inaunganisha miji maarufu ndani ya Tanzania na miji muhimu ya Lusaka na Harare. Sio marazote tunakuwa na Matokeo mazuri zaidi wakati mwingine tunakuwa na changamoto na tunashindwa kutoa huduma ambayo wateja wanategemea, ila daima tutajitahidi kuhakikisha kwamba Matokeo ya shughuli zetu ni mazuri na yanayoridhisha wateja.

Mbogoro anasema, shirika sasa linafanya kazi kwa bidii kuhakikisha kwamba wateja wanapata huduma bora kabisa wanaposafiri na fastjet. “Timu yetu mpya ya huduma kwa wateja imejidhatiti katika kuhakikisha mteja nakuwa na furaha kwa kila huduma anayopata wakati wa kuandaa safari hadi kufika aendako” Fastjet tayari imeshazindua huduma mpya ya vifurushi vya safari ambavyo ni Okoa pesa ambayo ina bei rahisi zaidi na haijumuishi mzigo wa kuingia chini ya ndege na kifurushi cha pili kinajulikana kama Safiri kijanja, ambacho ni nafuu pia na kinakupa begi moja bure, na uwezo wa kubadili tarehe ya safari au njia ya safari. “Fastjet ni shirika la watanzania wote, na tumejikita kuhakikisha tunaleta usafiri wa kuaminika, nafuu na salama”