Fastjet yatambulika kama shirika la ndege lenye thamani bora Afrika kutoka 2018 Air Transport Awards

Uingereza: fastjet imetambuliwa kama shirika la ndege lenye thamani bora Afrika mwaka 2018 kutoka Air transport awards hivi karibuni. Tuzo hizi zinazofanyika kila mwaka, zimetengenezwa na shirika la habari za usafiri linaloongoza kimataifa, ambalo huwa linatambua ubora wa huduma kutoka kwenye mashirika yote yanayofanya shughuli za usafirishaji wa njia ya anga duniani. Tuzo hii ni ya tatu kwa fastjet huku ikiwa na tuzo nyingine kama Skytrax World Airline Awards’ Best Low-Cost Airline ndani ya Afrika na the World Travel Awards’ Leading African Low-Cost Carrier zilizotolewa mwaka 2017.

"Ni heshima kubwa kupokea tuzo hii kutoka kwa shirika kubwa kama hili ndani ya sekta yetu" alisema Mkurugenzi mkuu Nico Bezuidenhout. "Pia tuzo hii inatupatia matokea chanya ya mabadiliko ambayo tumekuwa tukifanya ambayo yalijumuisha kubadili mfumo mzima wa mtandao wa safari zetu, kubadili aina ya ndege na mfumo mpya wa ukataji wa tiketi, ikijumuisha pia uzinduzi wa safari zetu ndani ya Msumbiji na kuhamisha ofisi nzima kutoka London kwenda kwenye ardhi ya Afrika" Bezuidenhout aliongeza kwa kusema tuzo hizi pia zinaonesha mchango wa wafanyakazi wa afastjet ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii ili kufanikisha shughuli zote kwenye mtandao wa ndege zetu na hii ikionekana hata kwenye kuondoka na kufika kwa wakati kwa ndege za fastjet kwa mwezi wa kwanza na wapili mfululizo. (Januari 91% na Februari 94%)

Akizungumzia tuzo hizi Heather Ryan muandaaji wa tuzo amesema: "Tuzo hizi zinatambua mashirika ambayo wafanyakazi wao wamechangia katika kuendeleza mafanikio ya sekta hii na kuwapa tuzo kutokana na juhudi yao katika kazi, ubunifu na mafanikio. Hivyo ningependa kutoa pongezi zangu za dhati kwenu kwa niaba ya International Transport News Magazine kwasababu mmstahili tuzo hii na tunawatakia mafanikio mema" International Transport News inajisifu kwa kuchagua washindi halali na huku tukitoa tuzo kwa washindi wanaostahili kweli kutokana na kufanya kazi kwa bidii na kujitofautisha kwao kutoka kwa washindani wao huku wakionesha kuwa wanastahili kutambulika.