Kwanini usafiri na basi wakari unaweza kuruka na ndege kwa bei nafuu kutoka Dar kwenda kigoma?

Tunapenda kukuona ukitembelea ndugu, jamaa na marafiki au ukitembelea kujionea uzuri wa asili wa Tanzania kwa Fastjet shirika ambalo linakupa bei nafuu za safari za ndege . Hii inamaanisha kuwa sasa unaweza kusema kwaheri kwa safari zote za basi na treni zinazotumia muda mingi njiani. Furahia kusafiri na Fastjet kwa kuruka kwa dakika 90 tu.

Unapokata nauli ya bei nafuu na fastjet unakuwa na uwezo wa kusafiri kote Tanzania ili ukasalimie wapendwa wako au kwa nia tu ya kufurahia uzuri wa asili wa Tanzania. Unasubiri nin? kata tiketi yako sasa kwa bei ya kuanzia 123,000 tu kwa safari kati ya Dar es salaam na Kigoma. Bado Huamini? Twendezetu tukafurahie safari yetu kutoka Dar es salaam kwenda Kigoma.

Matangazo machache ya Kiswahili yakifuatiwa na kingereza huku  kwa muda mfupi kidogo yakiingiliana na maongezi ya abiria waliokuwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam. Muda ulikuwa umefika wa sisi kuanza safari ndani ya ndege kutoka Dar es salaam kwenda Kigoma, Mkoa ambao unapatikana magharibi mwa Tanzania. Safari ya saa 1.40 ilitufikisha kwenye mji mzuri wa Kigoma baada ya kusafiri umbali wa maili 676 au Km 1088.

 

Uwanja wa ndege wa Kigoma

Nilishuka Uwanja wa ndege wa Kigoma , na abiria mwenzangu aliniuliza kwanini nilipenda kusafiri kwenda Kigoma. Bila hata ya kufikiri nilisema “Kwaajili ya uzuri wake na Historia”. Kama nilivyotarajia, kigoma haikuniangusha.

Serikali inategemea kufanya upanuzi wa jengo wanalotumia abiria kusubiria ndege na baadae barabara inayotumika kuruka ndege.

 

Hali ya hewa ikoje?

Kigoma has a tropical savanna climate, with an average temperature of 23.3 degrees C. November is the coolest month. On average, the rainy season is from November to April, with March being the wettest. June to September are the dry months, with July being the driest.

Kigoma ina hali ya hewa ya kitropiki ya savanna, na joto la kawaida la digrii 23.3 C. Novemba ni mwezi wa baridi zaidi. Kwa wastani, msimu wa mvua unatoka Novemba hadi Aprili, na Machi huwa ni mwezi wenye mvua pia. Juni hadi Septemba ni miezi ya kiangazi, na Julai huwa na jua kali zaidi.

 

Vipi kuhusu malazi kwenye mji wa Kigoma?

Unaweza kupata nyumba za wageni nzuri ndani ya mji wa Kigoma ambazo ziko kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika. Furahia faragha yako binafsi ya pwani, huku ukifurahia kuona punda wanaokuja kunywa maji ya ziwani. Mji huu pia una mitende mingi iliyotawanyika kote, hii inaufanya mji huu kuwa kama Paradiso. Samaki wadogo wanaweza kuonekana wakiogelea karibu na pwani ya ziwa huku wakionyesha rangi zao nzuri.

 

Mji wa Kigoma

Ikiwa imezungukwa na milima na misitu, Kigoma inaangalia pwani ya mashariki ya Ziwa Tanganyika. Kigoma ina bandari ya ziwa na mji uliochangamka ambao uko magharibi mwa Tanzania. Ni kilomita 60 kutoka mpaka wa Burundi hadi kaskazini. Mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) unagawanya Ziwa Tanganyika katikati kutoka kaskazini hadi kusini, na iko karibu kilomita 25 magharibi mwa mji. Mji uko chini ukiwa na uinuko wa mita 775 tu.

Mji huu ulishawahi kuwa kituo maarufu cha biashara. Mji hu pia una kituo cha zamani cha reli, kilichokuwa cha mwisho kwenye reli ambayo iliunganishwa na Dar es Salaam. Historia ya kikoloni ya Ujerumani inaonyeshwa katika Nyumba ya Kaiser (KaiserHouse), pamoja na majengo mengine ya wakati huo huko Kigoma.

 

Makumbusho ya Livingstone Kigoma

Kwanini usitembelee makumbusho ya kuvutia zaidi, yaliyojengwa mahali ambapo Livingstone na Stanley walikutana chini ya mti wa muembe. Uwekaji wa chuma kwenye ukuta wa makumbusho unasema hivi: "Chini ya mti wa muembe ulio simama hapa, Henry M. Stanley alikutana na David Livingstone 10 Novemba 1871."

 

Lake Tanganyika

Simama kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika, na utaona kwamba umbali ambao jicho linaweza kuona, utaona maji tu. Ni kama bahari, isipokuwa hakuna mawimbi halisi, na ni maji safi (ingawa ni brackish) kinyume na maji ya bahari. Ziwa Tanganyika lina urefu wa kilomita 660 ni ziwa lenye maji safi zaidi duniani, na la pili ya kina, baada ya Ziwa Baikal la nchini Urusi. Upana wake ni  kilomita 17 hadi 72 km, na lina ukubwa wa eneo la karibu kilomita 33 za mraba. Ziwa liko katika sehemu ya kusini ya Bonde la Ufa upande wa Magharibi.

Kuchukua fursa hii kufanya safari ndani ya Ziwa Tanganyika kutoka bandari ya Kigoma, kwa kupanda kwenye boti la zamani la abiria duniani. Meli hii ya mvuke, inayoitwa MV Liemba, ilijengwa huko Hapsburg, Ujerumani, mwaka wa 1913. Inatoka mara moja kwa wiki kutoka Kigoma, ikitembea katika miji kadhaa ya Tanzania, na hatimaye kufika eneo la kusini la Ziwa, huko Mpulungu, Zambia. Ni safari ya siku 5 yenye juml ya kilomita 1144. Ambapo hakuna bandari, abiria hutoka katika boti ndogo. MV Liemba pia inaweza kukushusha kwenye bandari ya Kipili.

 

Ujiji

Karibu kilomita 10 kusini mwa Kigoma ni mji wa kale kabisa kaskazini mwa Tanzania unaoitwa Ujiji. Kihistoria una maslahi makubwa, kwa sababu hii ndio sehemu ambapo Henry Stanley alikutana na Dk David Livingstone tarehe 10 Novemba 1871, na akasema maneno haya yatakayoishi milele, "Natumaini wewe Dr Livingstone".

 

Gombe National Park

Ikiwa una nia ya kutembelea sokwe maarufu aina ya chimpanze ambao ilifanyiwa utafiti na Jane Goodall, basi Gombe National Park ni sehemu sahihi ya kutembelea. Hifadhiina ukubwa wa kilomita 10 kaskazini mwa Kigoma na inapita kando ya milima kwenye pwani ya mashariki ya Ziwa Tanganyika. Inapatikana tu kwa mashua. Mbali na chimpanzi, pia kuna aina ya ndege zaidi ya 200.

Kwa hiyo, bei nafuu inaweza dhahiri kuwa na furaha lakini endapo tu utasafiri na fastjet. Ruhusu fastjet ikusafirishe kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kwa gharama nafuu. Ni mara 3 kwa wiki na kila mtu atafurahia.

 

Sources:

1 https://www.tripadvisor.com/Hotel_Review-g660803-d1501705-Reviews-Jakobsen_s_Beach_and_Guesthouse-Kigoma_Kigoma_Region.html

2 https://en.wikipedia.org/wiki/Kigoma

3 https://weather-and-climate.com/average-monthly-Rainfall-Temperature-Sunshine,Kigoma,Tanzania

4 http://www.weatherbase.com/weather/weather-summary.php3?s=10836&cityname=Kigoma%2C+Kigoma%2C+Tanzania&units=

5 https://weather-and-climate.com/average-monthly-Rainfall-Temperature-Sunshine,Kigoma,Tanzania

6 https://www.tripadvisor.co.za/Attraction_Review-g660803-d3190370-Reviews-Livingstone_Museum_Memorial-Kigoma_Kigoma_Region.html#REVIEWS

7 https://www.enchantingtravels.com/destinations/africa/tanzania/kigoma/

8 https://www.tripadvisor.co.za/ShowUserReviews-g293747-r35138552-Tanzania.html

9 https://en.wikivoyage.org/wiki/MV_Liemba