Safiri na fastjet kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya kwa bei nafuu!

Gundua uzuri wa asili wa Tanzania au washangaze wapendwa wako – ni rahisi na nafuu, unapokata tiketi za bi nafuu na Fastjet kutoka Dar es salaam kwenda Mbeya. Kwa bei ya kuanzia tsh 87800, Fastjet itakupeleka kwa haraka na kwa raha mustarehe. Mbeya itafanya safari yako kuwanzuri nay a kukumbukwa.

Karibu dakika 30 kabla ya jua kuchomoza, hewa ya joto la Dar es Salaam tayari ilianza kutukumbatia wakati tunatoka kwenye hoteli yenye kiyoyozi kuelekea  uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Tulipoingia uwanja wa Ndege tayari kwa safari ya kwenda Mbeya, tulifikiria siku chache nzuri tulizofurahia jijini Dar es Salaam. Dar es Salaam, inayojulikana kama Mzizima au 'Healthy Town' kwa Kiswahili, imetoka kwenye neno la Kiarabu la Dar as-Salam, ikimaanisha "nyumba ya amani." Mji ulijengwa kwanza mnamo 1866, chini ya Sultan Majid bib Said wa Zanzibar. Kama mji mkuu wa zamani wa Tanzania mpaka mwaka wa 1974, ni jiji la watu wengi wanaozungumza Kiswahili nchini Tanzania.

Lakini, hiyo ilitosha – tuliamua kuweka akili yetu kwenye maajabu ya safari yetu ndani ya Tanzania kwa kutembelea Mbeya. Safari ya kilomita 817 kwa barabara inaweza kufunikwa katika masaa 11. Hata hivyo, kuruka hupunguza umbali na huchukua dakika 85 tu

Tulifurahi sana kupanda ndege ya fastjet, na haikuchukua muda tukasema kwaheri kwa jiji la Dar es Salaam.

Tulipaa juu urefu mkubwa, dakika 25 kabla ya kutua uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, kilomita 20 kutoka mji wa Mbeya. Ndege iliruka juu A104 usawa wa barabara kuu inayoingia jijini Mbeya, nilichungulia chini kupitia dirishani na kwa mbali niliona jiji la Mbeya iliyopotoka chini.

Tangazo la wafanyakazi wa ndani ya ndege la kukaribia kuwasili katika Uwanja wa Ndege ilivunja hali ya utulivu, huku abiria wachache waliokuwa wamelala wakiinua vichwa Kuangalia nje ya dirisha, huku Jiji la Mbeya likitusalimu kwa mbali. Baada ya muda mchache, ndege ilitua na magurudumu yake yaligusa barabara.

Unaweza kuuliza, kwanini mtu atembelee Mbeya? Kuna sababu nyingi nzuri, muhimu zaidi ni kupata uzuri wa ajabu wa milima, maziwa, misitu na mimea.

 

Jiji la Mbeya

Ukiwa na urefu wa mita 2,656 mlima Loleza ulioko jijini Mbeya, jiji lililoko karibu kilomita 60 kaskazini mwa Usungu Game Reserve, na karibu kilomita 80 upande wa magharibi na Uwanda wa Game Reserve, ulioko kando ya Ziwa Uwanda

Mnamo miaka ya 1920, Mbeya ilianzishwa kama mji wa madini ya dhahabu baada ya kugudulika kwa dhahabu mwaka 1905. Aidha, wajasiriamali wengi waliishi eneo hilo wakati reli ya TAZARA ilipofunguliwa.

Leo, Jiji la Mbeya linaunda kanda za biashara kwa wilaya za kusini za Tanzania na nchi za jirani za Kongo, Zambia, na Malawi. Jiji iko kwenye barabara kuu ambayo inaungana na 'barabara kuu ya Kaskazini,' ambayo inatoka Cape Town kwenda Alexandria.

Eneo ambalo linazunguka Mbeya limeitwa 'Scotland of Africa', linalothibitishwa na milima iliyofunikwa na heather na bracken, ambayo pia inafanana na fynbos ya Western Cape.

 

Ngozi Crater Lake

Kwanini usiende kutembelea Ziwa la Ngozi, liko  umbali wa kilomita 38 kusini mwa Mbeya, na liko katika Hifadhi ya Misitu ya Mporoto. Hili ni ziwa kubwa la pili Afrika linalopatikana kwenye caldera au ukanda wa volkano, na lina ukubwa wa kilomita 2.5, urefu wa kilomita 1.5, na kina cha mita 300. Tembea msituni, na uangalie nyani na aina mbalimbali za ndege wazuri.

Kitulo National Park

Karibu kilomita 120 au saa 1.5-hr kwa gari unapotoka Mbeya ni Hifadhi ya Taifa ya Kitulo. Wakazi waliiita 'Bustani ya Mungu'. Eneo hilo lina mimea na maua mbalimbali kama, aloes na orchids. Sababu eneo hili la hifadhi ni dogo hapa ndipo utamaliza kiu yako ya kuona madhari nzuri na ya ajabu.

Milima ina urefu zaidi ya mita 2,500. Kama una nguvu za kutosha unaweza kupanda hadi kileleni, kupitia Milima ya Livingstone, na kushuka chini kwenda hadi Matema Beach kwenye Ziwa Nyasa, au Ziwa Malawi kama linavyojulikana.

 

Pumzika kwenye fukwe nzuri za Matema Beach

Kwenye safari  hii itapita vilima na vijiji mbalimbali, kisha utafika Matema Beach, kilomita 130 kutoka Jiji la Mbeya. Ni fukwe yenye mchanga mweupe mzuri, na iko kwenye ncha ya kaskazini mwa Ziwa Malawi. Chukua boti ikuzungushe na ufurahie utulivu wa ziwa hili.

Nunua sasa tiketi yako na shirika la ndege lenye gharama nafuu kati ya Dar es Salaam na Mbeya kwa safari za kila siku kwa wote.

 

Sources:

1 https://en.wikipedia.org/wiki/Dar_es_Salaam

2 https://www.distancecalculator.net/from-dar-es-salaam-to-mbeya

3 https://en.wikipedia.org/wiki/Mbeya

4 https://en.wikipedia.org/wiki/Loleza_Mountain

5 http://www.sisi-kwa-sisi.com/attractions.html