Sehemu 5 za kufanya Shopping ukiwa Dar es Salaam

By Candice de Beer

Afrika ni sehemu nzuri Zaidi ya kujipima uwezo wako wa kumpunguzia bei muuzaji na upeleke nyumbani zawadi nzuri au vitambaa uvipendavyo. Hizi ni sehemu 5 tunazoshauri utembelee ukiwa Dar es Salaam.

Mwenge Vinyago
Ukiwa Afrika hauhitaji kusafiri umbali mrefu kutafuta vinyago vilivyochongwa vizuri kabisa. Vinyago hivi vinakuja katika shepu mbalimbali  na saizi. Hufungwa vizuri na utasafiri navyo salama, ukifika nyumbani utaviweka kwenye kabati lako na kupendezesha nyumba yako. Vinyago hivi pia hudumu kwa muda mrefu kama havitawekwa kwenye mazingira magumu na vitakukumbusha safari yako ndani ya Afrika. Utapata vitu vingi vitakavyokuvutia na vyenye rangi ya kuvutia utakapokwenda Mwenge Vinyago. Njoo na pesa taslim na kaa tayari kuomba kupunguziwa bei.

Tingatinga Art Centre
Hivi pia ni maarufu sana Tanzania, ni mtindo wa kupaka rangi wa Tinga tinga. Mtindo huu ambao hutokana na kutumia rangi za mafuta na kutengeneza michoro ya katuni, huvutia sana. Usiondoke Dar es salaam kabla haujanunua Tingatinga na uweke kwenye frem ufikapo nyumbani. Utapata aina nyingi hapa Tingatinga Art Centre.

Soko la Kariakoo
Ukitaka kwenda sehemu ambayo utafanya manunuzi ya kiafrika nenda Kariakoo – Hili ni soko kubwa na maarufu Zaidi Dar es salaam. Hapa utapata kila kitu, kuanzia vyakula, rangi, nguo na vito. Muuzaji anategemea uombe kupunguziwa bei kwahiyo usikubali kununua kitu kwa bei ya kuanzia. Pia tunashauri uende mapema. Ukienda muda ambao soko limejaa watu huwezi pata vitu kwa bei nzuri.

Soko la samaki la Ferry 
Kama unapenda samaki fresh, nenda soko la samaki la ferry ili upate samaki wazuri Zaidi wa siku hiyo hiyo. Soko hufunguliwa saa 630 asubuhi na hutumiwa na watu mbalimbali toka kila kona ya jiji. Mnada ukishaanza unaweza ukapata wakati mgumu kupata samaki uwatakao lakini kama umependa samaki hao usiogope kutoa bei yako. Haijalishi utawanunua kwa bei gani lakini nakuhakikishia samaki hawa freshi ni watamu sana.

Maduka ya kanga ya mtaa wa Uhuru
Kama unapenda vitambaa vyenye rangi ang’avu unahitaji kanga katika Maisha yako. Hizi zinapatikana katika kila aina ya rangi, kuna nzito na nyepesi na unaweza kutengenezea vitu mbalimbali kama kava za mito ya makochi, Kofia. Chukua taxi hadi sehemu hii na fanya manunuzi yako. Usisahau kuomba punguzo la bei wanuzaji wanapenda.

Ushauri wetu
Kabla hujaenda popote tunashauri uvae nguo za kawaida usijioneshe utajiri wako. Kama una vitu vya thamani kama saa au vito vifungie hotelini unayokaa. Vibaka wapo na huwa wanaangalia mtu ambaye wanaweza kumuibia na kukimbia.

Safiri na fastjet
Kam Dar es salaam ndo jiji unalotarajia kwenda  kwaajili ya likizo yako ijayo, chagua fastjet ikupeleke huko. Ikiwa ni kampuni ya ndege yenye bei ambazo kila mtanzania anaweza kuzimudu, itahakikisha inakupeleka kwenye miji yote mikubwa ya Tanzania. Angalia ramani yetu ya safari ili kuona unaweza kusafiri wapi na sisi. Pia unaweza kukata tiketi yako sasa.