Kutana na Magdalena Sanga mfanyakazi bora kitengo cha biashara mwaka 2017

1/18/2018 9:00:00 AM

“Nimehamasika sana. Asante sana shirika langu la fastjet kwa kunipatia tuzo ya Mfanyakazi bora kitengo cha biashara kwa mwaka 2017 pamoja na zawadi ya tiketi ambayo nitaitumia kwenda Mbeya kusalimia wazazi wangu, ndugu, jamaa na marafiki. Najivunia shirika langu.“

 

Magdalena Sanga anafanya kazi kama afisa mauzo wa shirika la ndege la fastjet tangu mwaka 2015, kwa sasa anafanya kazi katika ofisi ya Samora iliyopo jijini Dar es salaam, awali alifanya kazi katika ofisi ya fastjet makao makuu na katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.

 

Akipokea tuzo hiyo alisema; “Tuzo hii imenipa motisha mpya mimi pamoja na wafanyakazi wenzangu kufanya kazi kwa uaminifu na kwa bidii zaidi ili kutoa huduma bora kwa wateja wetu wazidi kutuamini kila siku.” 

 

Akizungumza katika utoaji tuzo huo, Christine Kausan, msimamizi wa kitengo cha biashara ofisi ya fastjet Dar es Salaam alisema, “Tuzo hii itawapa motisha wafanyakazi wengine kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Magdalena ni mchapakazi, anawahi kazini, anafanya kazi bila kusimamiwa, anajua sheria za kampuni na ni mzoefu wa kutatua matatizo ya wateja. Magdalena anatoa msaada mkubwa pia kwa wafanyakazi wenzake.”

 

Kitengo cha biashara kina ofisi Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza, kazi kubwa ya kitengo cha biashara ni kuuza tiketi kwa wateja, kutoa ushauri kuhusu bidhaa za fastjet, kuhamasisha wateja watumie bidhaa za fastjet ambazo ni nafuu na rahisi pamoja na kuhamasisha makampuni yaungane na fastjet kupata huduma bora zaidi.

 

Karibuni wateja wetu katika ofisi zetu mbalimbali kwa huduma bora na tiketi za gharama nafuu.

 

fastjet kwa wote

 

By Bill Marwa - @BillMarwa