Best African Low-Cost Airline Africas leading low cost airline 2016 winner shield Book Direct for the Lowest fares

Uhakika wa bei kwenye mtandao Nunua tiketi yako moja kwa moja kupitia www.fastjet.com kwa ajili ya kuepuka ada za ziada

Maswali ya mara kwa mara

1. Ofisi zenu zipo wapi? Na muda wa kufungua na kufunga ofisi ni upi?

Unaweza kupata orodha ya ofisi zetu na muda wa kazi kwenye: http://www.fastjet.com/tz/sw/contact/fastjet

2. Ni lini mtaanza safari zenu mpya na mtapaa kuelekea wapi?

Tunaendelea kutanua wigo wa safari zetu – baada ya kuanza kuruka kuelekea Afrika Kusini kati ya Johannesburg na Dar Es Salaam na pia safari za Zambia kati ya Lusaka na Dar Es Salaam, tumejizatiti na kuweka mipango kwa ajili ya kupanua huduma zetu katika nchi nyingi barani Afrika. Safari mpya zitakuwa zikitangazwa kupia tovuti yetu, ukurasa wa facebook, twitter na kupitia magazeti na radio. Endapo utapenda kupata habari kwa haraka kuhusu mpango wetu kutanuka na kuwa wa kwanza kujua kuhusu safari mpya jiunge kwenye gazeti letu la mtandao http://www.fastjet.com/tz/sw/signup

3. Kwa nini mnatoza mizigo na ni kiasi gani mnatoza?

Kama ilivyo kwa huduma nyingine za mizigo, wateja wetu wa mara kwa mara huwa wanafaidika na burudani mbalimbali wanapotumia fastjet,ndege ya bei nafuu kuliko nyingine.

Unaweza kusafiri na begi moja tu la mkononi, ambalo ni bure, na kama litakuwa kubwa sana utalipakia kama mizigo mingine.

Tafadhali ona gharama a zetu na ada katika http://www.fastjet.com/tz/sw/plan-your-trip kwa kupata habari zaidi.

4. Kwanini nauli zinabadilika?

Nauli za fastjet huongezeka mteja anapofanya maandalizi ya safari siku chache kabla ya safari, sababu ni kwamba wale wanaofanya maandalizi ya safari zao siku mchache kabla ya safari, wanakuwa katika wakati mgumu wa kupata bei ya chini na hupungua anapofanya maandalizi mapema.

Kwa maana hiyo wanaochelewa kununua tiketi wanapata nauli ya bei juu kuliko wale walionunua mapema.

5. Nawezaje kupata bei mpya za nauli?

Nauli zetu mpya zote zinapatikana katika tovuti yetu ya fastjet.com, na katika,simu yako utaipata m.fastjet.com, itakupa mwongozo mzuri wa kutafuta ndege zetu na bei zetu.

Kwa wale ambao hawana kompyuta, mtandao wetu wa simu za mkononi m.fastjet.com unakupa fursa sahihi ya kutafuta ndege na nauli.

6. Nalipa vipi kwa njia ya mtandao wa simu? 

Malipo kwa njia ya mtandao wa simu yanapatikana Tanzania, Kenya na Uganda na inafanya kazi sawa kama vile unavyolipia umeme.

Fuata njia hizi kulipia safari yako ya ndege na fastjet kwa kutumia njia ya mtandao wa simu:

 1. Ukishachagua tarehe yako ya safari na huduma nyingine za ziada, unaweza kuingiza majina na nambari za mawasiliano za mteja kwa uangalifu wakati unaponunua tiketi.
 2. Kisha chagua "Lipa sasa kwa kutumia mtandao wa simu" kwenye menyu yako.
 3. Hakikisha umesoma na kukubaliana na vigezo na masharti kabla hujabonyeza mbele kwenda kurasa ya malipo.
 4. Ukishabonyeza 'next' utapewa dakika 15 ili kulipia tiketi yako. Hakikisha una hela ya kutosha kwenye akaunti yako ya simu.
 5. Tafadhali chagua nchi gani ungependa malipo yako yafanyike.
 6. Ukishachagua nchi, utapata njia mbalimbali za kulipia tiketi kwa njia ya simu yataonekana, na ukibonyeza kwenye chaguo moja wapo utapata maelekezo ya jinsi ya kulipia.
 7. Utapokea SMS yenye kodi ya uhakiki kutoka kwenye kampuni ya simu. 
 8. Ingiza hii kodi ya uhakiki amoja na namba yako ya simu na bofya 'compleate'

Endapo itatokea malipo yako kamili hayajapokelewa wakati unalipa tiketi yako, tiketi itasitishwa na nauli inaweza kubadilika pindi utakaponunua tena tiketi.

Pindi maipo kamili yakipokelewa fastjet itakutumia ujumbe wa uhakiki na kukutumia tiketi yako kupitia barua pepe 

Vigezo vya utumiaji: Endapo itatokea umefanya malipo kwa bahati mbaya, utarudishiwa pesa yako kwa njia ya simu bila kuchajiwa na mtoa huduma wako, PesaPal.

7. Je naweza kubadilisha tiketi yangu na kulipia gharama zote kwa njia ya mtandao?

Inawezekana kubadilisha tiketi yako kwa kulipia gharama zote zinazotakiwa kwa kupitia mtandao wetu wa fastjet.com na katika simu yako pia, m.fastjet.com kwa kuingia katika kipengele cha "simamia mpango wangu wa safari". Kama unatumia M-Pesa au Tigo pesa unapaswa kulipia mara tu baada ya kubadilisha tiketi yako.

8. Je nahitaji kuwa na kitambulisho changu wakati ninaposafiri kwa fastjet?

Unahitajika kubeba kitambulisho chako unaposafiri safari za hapa hapa ndani ya nchi, na unaposafiri safari za kwenda nchi za nje kama Afrika ya kusini au Zambia, utahitajika kubeba  Pasi yako ya kusafiria.

9. Je huwa mnakubali kuunganisha na ndege nyingine?

Tunawapa wateja wetu chaguo la kuunganisha safari zao za ndege kupitia kituo chetu kikuu cha ndege cha Dar es Salaam. Kwamfano utakapotaka kusafiri kutoka Harare kwenda Kilimanjaro, utapanda ndege mbili tofauti zenye namba mbili tofauti za ndege. Utasafiri kwanza kutoka Harare kwenda Dar na kasha utatoka ndani ya ndege na kuingia tena uwanja wa ndege ambapo utajitambulisha kwenye dawati letu la ukaguzi mwakilishi wetu atakuelekeza pa kupita kasha utasafiri na ndege nyingine kutoka Dar es Salaam kwenda Kilimanjaro. Ndege za kuunganisha zina faida kadhaa:

 • Wavuti yetu ya www.fastjet.com inakupa chaguo bora zaidi la kuunganisha safari yako. Ni rahisi chagua sehemu unazotaka kusafiri na tarehe, na wavuti yetu itakupa chaguo bora zaidi.
 • Safari zako zote zinaweza kufanywa kwa pamoja kwenye namba moja ya kumbukumbu.
 • Utalipa kodi kwa safari ya kwanza katika zile unazounganisha.
 • Utalipa mzigo mara moja.
 • Fastjet itahakikisha kwamba wateja wote watakaonunua tiketi za kuunganisha wanafika kwenye vituo vyao vya mwisho. Endapo kutatokea kuchelewa kwa ndege fastjet itawahamishia wateja kwenye ndege ya fastjet inayofuata bila gharama yoyote. (Tafadhali angalia vigezo na masharti kwa maelezo zaidi).

Tafadhali tambua kwamba safari ya kuunganisha na safari ya mojakwa moja ni vitu viwili tofauti. Kwa mfano, ndege ya kutoka Dar es Salaam kuelekea Entebbe ni safari ya moja kwa moja lakini inakituo kimoja ambacho ni Kilimanjaro. Abiria watasimama Kilimanjaro wakiwa safarini, lakini watabaki kwenye ndege. Na safari hii yote ina namba moja ya ndege.

10. Je ni salama kusafiri kwa kutumia fastjet?

Katika ndege zetu, usalama ni wa uhakika. Kama ilivyo afya kwa wafanyakazi na abiria wetu, ndio maana fastjet tuna ndege za kisasa, kama ndege yetu kubwa aina ya airbus A319s, inayofanya kazi katika viwango vya kimataifa vya usalama, na katika technolojia. Inaweza kubeba abiria 156, na wahudumu wetu wa ndege waliobobea na kupitia mafunzo ya hali ya juu katika kila ndege na pia tuna mafundi wa hali ya juu kwa ajili ya kufanya marekebisho.

Kama mazingira yanavyoruhusu usafiri wa anga, fastjet inarusha ndege za kisasa katika ambazo hazina madaraja ya kibiashara wala lile daraja la kwanza.

Kwa maana hiyo, fastjet ina mtandao mzuri wa bei rahisi kwa wateja wake katika nchi za afrika mashariki.

11. Je huwa mnatoa viburudisho katika ndege zenu?

Fastjet hutoa viburudisho katika ndege zetu za hapa nchini na nje ya nchi, hutoa viburudisho vya moto, baridi na vile vyenye vilevi pia kulingana na mahitaji ya mteja wetu. Mlo kamili na bei zake hupatikana hapa. Angalia prodha ya vyakula na bei zake

12. Ndiyo Fastjet wanaweza kubeba shehena?

Fastjet  tunashirikiana na BidAir Cargo, ambao ni mawakala wa kubwa wa kubeba shehe Afrika. Kwa maelezo zaidi au kulipia nafasi ya shehena wasiliana na Lilian Olweni at BidAir:  liliano@bidaircargo.com.

13. Naweza kununua mapema siti ninayopenda?

Ndio,katika kila ndege yetu ya Fastjet unanafasi  ya kuchagua siti kwa bei ya chini pale unaponunua  kwa njia ya mtandao au kupitia huduma kwa wateja. Tunatoa nafasi ya ziada kuweka miguu pamoja na siti za kutoka kwa haraka kwa gharama ya Dola 5 na siti zingine kwa gharama ya Dola 3.

14. Siti zilizokatwa mapema gharama zinarudishwa na kama ndio, ni nani nahitaji kuwasiliana naye?

Siti zilizolipiwa tayari gharama hazirudishwi. Pale inapotokea kwa bahati mbaya tumefuta safari kwenye ndege ambayo ulichagua siti, utatakiwa kurudishiwa gharama zote ulizolipa au kuhamishiwa kwenye siti ya karibu na ile uliyolipia.Tafadhari wasiliana na watoa huduma wetu kwa msaada.