Best African Low-Cost Airline Africas leading low cost airline 2016 winner shield Book Direct for the Lowest fares

Uhakika wa bei kwenye mtandao Nunua tiketi yako moja kwa moja kupitia www.fastjet.com kwa ajili ya kuepuka ada za ziada

Jinsi ya kununua tiketi kwenye mtandao

Kununua tiketi kupitia mtandao wetu ndio njia rahisi kabisa ya kupata nafasi kwa ajili ya safari za fastjet. Unaweza kupata punguzo la bei la hivi karibuni kabisa; pata habari kuhusu bei zetu za chini kabisa na uepuke kulipia ada za mawakala.

Kununua tiketi ukitumia mtandao wetu fuata hatua zifuatazo:

 1. Angalia uwepo wa nafasi

  Ingiza taarifa kuhusu utokako, uendako, tarehe za kusafiri na idadi ya wasafiri kwenye kisanduku cha ‘nunua tiketi’ kilichopo kwenye upande wa kushoto wa mtandao. Bofya ‘endelea’ kuona uwepo wa nafasi.

 2. Chagua pendekezo lako la ndege

  Nauli zote zilizopo kwenye tarehe ulizochagua zitaonekana kwenye upande wa kulia wa kioo. Ili kuona ndege kwenye tarehe nyingine tafadhali bofya vitufe vya ‘mapema na baadae’ kwa ajili ya ndege zinazoingia na zinazotoka.

  Mara upatapo ndege unazozitaka, tafadhali zichague kwenye upande wa kulia wa kioo na ubofye ‘endelea’.

  Endapo kwa bahati mbaya umechagua ndege ambazo sizo unaweza kufuta kikapu chako upande wa kushoto kioo unaweza kuboresha utafutaji wako kwa kuchagua upya utokapo, uendako, tarehe za safari na idadi ya wasafiri.

 3. Ingiza taarifa za msafiri

  Kama umeridhika na muda wa safari na nauli ulizochagua, bonyeza ‘endelea’.

 4. Thibitisha safari

  Jaza taarifa zote muhimu za wasafiri wanaosafiri kwenye tiketi yako. Majina lazima yafanane sawia na yale yaliyoko kwenye hati au nyaraka za kusafiria za wasafiri. Jaza taarifa zako za mawasiliano na tufahamishe iwapo una mahitaji yoyote maalumu.

  Ili kuendelea na hatua inayofuata ya kununua tiketi, thibitisha kama umesoma na unakubaliana na vigezo na mashartiya kampuni kabla ya kubonyeza ‘endelea’.

 5. Uthibitisho na malipo

  Ukishathibitisha taarifa za wasafiri wote utatakiwa kuchagua njia ya malipo. Unaweza kulipia safari yako kwa kutumia njia yoyote kati ya hizi zifuatazo:

  • Credit Card au Debit Card
  • M-Pesa
  • Tigo Pesa
  • Kwa pesa taslimu kaunta au kwa Credit card kwenye ofisi yoyote ya fastjet

  Kama unalipia katika ofisi za fastjet au wakala, malipo yanapaswa kufanywa ndani ya muda muafaka, yaani ndani ya

  • Masaa 48 kama unasafiri ndani ya mwezi
  • Masaa 24 kama unasafiri ndani ya siku 4
  • Masaa 6 kama unasafiri chini ya siku 4
  • Saa 1 kama unasafiri ndani ya masaa 24

  Ukiwa unachagua aina ya malipo utapokea namba ya kumbukumbu ya tiketi. Tumia namba hiikufanya malipo kama ni katika ofisi ya fastjet au kwa wakala.

  Kama malipo hayatapokelewa ndani ya muda muafaka, nafasi ya safari itafutwa na hatutaweza kukuhakikishia tiketi kwa bei ya awali.